Pata taarifa kuu

Wapatanishi wa mzozo wa Ukraine kutoka Afrika kuaanza kazi mwezi huu

NAIROBI – Ujumbe wa viongozi wa Afrika wanaojaribu kusaidia kupata suluhu ya vita nchini Ukraine, wanatarajiwa kuanza kazi hiyo katikati ya mwezi huu, imesema ikulu ya Afrika Kusini.

Nchi za Afrika zinajaribu kutafuta suluhu ya kumaliza vita nchini Ukraine
Nchi za Afrika zinajaribu kutafuta suluhu ya kumaliza vita nchini Ukraine AP
Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliopita rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alisema rais wa Urusi, Vladmir Putin na mwenzake wa Ukraine, Volodymry Zelensky, kwa pamoja walikubali kupokea ujumbe wa amani wa marais 6 kutoka Afrika.

Katika tarifa iliyotolewa na ikulu ya Pretoria, imesema kuwa, baada ya mkutano wa viongozi wa Afrika uliofanyika Jumatatu ya wiki hii, walikubaliana kwa pamoja kuzungumza na rais Putin pamoja na Zelensky ili kusitisha vita na kupata suluhu ya kudumu.

Bila ya kutaja tarehe rasmi ambayo viongozi hao watasafiri, tarifa hiyo imesema marais wote 6 wamethibitisha kuwa wako tayari kusafiri kwenda Ukraine na Urusi katikati ya mwezi huu.

Miongoni mwa marais wanaotarajiwa kusafiri ni pamoja na rais wa DRC, Misri, Senegal, Afrika Kusini, Uganda na Zambia, na kinachobakia sasa ni kwa mawaziri wa mambo ya nje kutoka kwenye mataifa haya kukutana ili kuandaa mpango kazi.

Nchi za Afrika ndizo zimeathirika pakubwa na kupanda kwa bei ya nafaka na biashara kutokana na vita hii

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.