Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Côte d'Ivoire: Laurent Gbagbo hatoweza kupiga kura katika uchaguzi wa mwezi Septemba

Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo ameondolewa kwenye orodha ya wapiga kura iliyochapishwa Jumamosi na hataweza kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Septemba 2, uamuzi ambao unakasirisha chama chake.

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara na mtangulizi wake Laurent Gbagbo, katika ikulu ya rais mjini Abidjan, Julai 27, 2021, wakati wa mkutano wao wa kwanza tangu mgogoro wa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010-2011.
Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara na mtangulizi wake Laurent Gbagbo, katika ikulu ya rais mjini Abidjan, Julai 27, 2021, wakati wa mkutano wao wa kwanza tangu mgogoro wa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010-2011. © REUTERS - Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

"Mchakato wa uchaguzi unapoteza uaminifu wake," ameshutumu afisa wa chama cha rais wa zamani wa Côte d'Ivoire.

Ikiwa Bw. Gbagbo aliachiliwa na Mahakama ya kimataifa ICC dhidi uhalifu wa kibinadamu uliofanywa wakati wa mzozo wa umwagaji damu baada ya uchaguzi wa 2010-2011, atasalia chini ya kifungo cha miaka 20 jela nchini Côte d'Ivoire kwa "wizi" wa Benki Kuu ya Mataifa ya Afrika Magharibi (BCEAO) mwaka 2011.

Licha ya msamaha uliotolewa na Rais Alassane Ouattara mwaka jana katika kesi hii, bado amenyimwa haki zake za kiraia na kisiasa.

Siku ya Jumamosi, wakati wa uchapishaji wa orodha ya wapiga kura mjini Abidjan, Sébastien Dano Djédjé, afisa mkuu wa chama cha African People's Party - Côte d'Ivoire (PPA-CI), kilichoundwa na Bw. Gbagbo, ameshutumu uamuzi "usio wa haki".

"Hii inatilia shaka uaminifu wa Tume Huru ya Uchaguzi (CEI). Mchakato wa uchaguzi unapoteza uaminifu," ameongeza kabla ya kuondoka kwenye hafla hiyo na wajumbe wa chama cha PPA-CI.

"Hatutupiani maneno kuhusu Laurent Gbagbo. CEI inatekeleza kile ambacho sheria inasema," amejibu mwenyekiti wa tume hiyo, Kuibiert Coulibaly.

Baadhi ya wapiga kura milioni nane wameintishwa kupiga kura tarehe 2 Septemba ili kuchagua serikali za mitaa na za majimbo nchini Côte d'Ivoire.

Wakati wa uchaguzi wa urais wa 2020, ghasia zilisababisha vifo vya watu 85 na 500 kujeruhiwa. Uchaguzi wa wabunge wa 2021 ulifanyika kwa utulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.