Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Chama cha Gbagbo chajiunga na Tume ya Uchaguzi nchini Côte d'Ivoire

Chama cha rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo kimejiunga na Tume Huru ya Uchaguzi (CEI), kwa mujibu wa sheria ya rais, hatua zaidi ya kutuliza hali ya kisiasa nchini Côte d'Ivoire kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Miezi michache baada ya kurejea Côte d'Ivoire, Rais wa zamani Laurent Gbagbo alizindua chama chake kipya cha kisiasa Oktoba 16 na 17 mjini Abidjan.
Miezi michache baada ya kurejea Côte d'Ivoire, Rais wa zamani Laurent Gbagbo alizindua chama chake kipya cha kisiasa Oktoba 16 na 17 mjini Abidjan. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Katika agizo hili, la tarehe 15 Februari lakini liliwekwa wazi Jumatano, Rais Alassane Ouattara alimteua naibu kiongozi wa Chama cha African Peoples' Party - Côte d'Ivoire (PPA-CI), Demba Traoré, kwenye Tume ya Uchaguzi, CEI.

Chama cha PPA-CI kilizinduliwa na Bw. Gbagbo mnamo mwezi Oktoba 2021, miezi michache baada ya kurejea Côte d'Ivoire baada ya kuachiliwa na mahakama ya kimataifa ambayo ilimhukumu kwa uhalifu dhidi ya binadamu katika mgogoro wa umwagaji damu wa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010. Ushiriki wake katika CEI ulikuwa moja ya mada ya mazungumzo ya kisiasa yaliyofanyika mapema 2022 ili kuimarisha "utamaduni wa kidemokrasia" nchini.

Mbali na uteuzi wa Demba Traoré, IEC imerekodi ujio wa mwanachama mwingine mpya, Dan Jules Démonsthène, uliopendekezwa na chama tawala, Rassemblement des Houphouëtistes pour la Démocratie et la Paix (RHDP).

Kwa hiyo sasa Tume ya Uchaguzi ina wajumbe 18: mwakilishi wa Rais wa Jamhuri, mmoja wa Waziri wa Mambo ya Ndani, sita kutoka mashirika ya kiraia, tisa kutoka vyama vya siasa, wakiwemo watano kutoka upinzani, na mwakilishi wa Baraza la Juu la Mahakama. ..

"Tunakubali kuingia huku (kwa Demba Traoré ndani ya CEI), hatua ambayo ilitarajiwa tangu mwisho wa mazungumzo ya kisiasa mwaka mmoja uliopita", msemaji wa chama cha PPA-CI, Justin Koné Katinan ameliambia shirika la habari la AFP. ambaye hata hivyo anazingatia kuwa tume ya uchaguzi bado haina usawa katika kuugemea upande wa utawala. "Chombo hiki lazima kirekebishwe kabisa na kuacha tabia yake ya upendeleo," aliongeza.

CEI ina jukumu haswa la kuanzisha na kurekebisha orodha ya wapiga kura, kuandaa uchaguzi na kuhakikisha matumizi madhubuti ya kanuni za uchaguzi. Uchaguzi ujao nchini Côte d'Ivoire, uchaguzi wa manispaa na mikoa, umepangwa kufanyika mwezi Oktoba na Novemba 2023. Uchaguzi wa urais unatarajiwa kufanyika mwaka wa 2025.

Tangu uchaguzi wa rais wa 2020, ambapo ghasia zilisababisha vifo vya watu 85 na 500 kujeruhiwa, dalili kadhaa za utulivu wa kisiasa zimeonekana nchini Côte d'Ivoire. Uchaguzi wa wabunge ulifanyika kwa utulivu Machi 2021, na wapinzani Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé walirejea nchini, baada ya kuachiliwa na mahakama ya kimataifa.

Bw. Gbagbo, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela nchini Côte d'Ivoire kwa "wizi" wa Benki Kuu ya Afrika Magharibi (BCEAO) wakati wa mgogoro wa baada ya uchaguzi wa 2010-2011, pia alisamehewa na Rais Alassane Ouattara mwezi uliopita wa Agosti. Pia alipokea mwanzoni mwa mwezi Januari malimbikizo ya malipo ya maisha yake ambayo yalitokana na yeye kama mkuu wa zamani wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.