Pata taarifa kuu
Ivory Coast - Siasa

Ivory Coast : Rais Ouattara akutana na watangulizi wake

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara amekutana na watangulizi wake Laurent Gbagbo na Henri Konan Bédié, ikiwa ni juhudi zake za kulipatanisha taifa hilo.

Henri Konan Bédié (kushoto) na Laurent Gbagbo (kulia) wakiwa na rais  Alassane Ouattara ,wakati wakitoa  taarifa kwa waandishi wa habari, Julai 14, 2022.
Henri Konan Bédié (kushoto) na Laurent Gbagbo (kulia) wakiwa na rais Alassane Ouattara ,wakati wakitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Julai 14, 2022. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Gbagbo na Konan amekutana na rais Ouattara katika ikulu ya rais na kufanya mazungumzo kwa zaidi ya saa moja.

Baada kikao hicho, Gbagbo amesema mkutano wa jana ulikuwa wa kuelezana ukweli kuhusu maswala muhimu ya kitaifa, na  kwamba wanataraji mkutano huo utakuwa na manufaa makubwa yatakayobadili upepo wa kisiasa nchini humo.

Mkutano wa jana ni sehemu ya mapendekezo ya serikali ya kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani ili kupunguza joto la kisiasa .

Rais Ouattara, amesema mikutano kama hiyo itaendelea kufanyika, akilenga kuchukuwa mapendekezo ya watangulizi wake na kuyafanyia kazi.

Viongozi hao watatu wamekuwa kwenye siasa za Ivory Coast kwa zaidi ya miaka 50, mkutano wa jana ukiwa wa kwanza kuwaleta pamoja mahasimu hao wa kisiasa tangu mzozo wa uliotumbikiza taifa hilo kwa mapigano mwaka 2010.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.