Pata taarifa kuu

Laurent Gbagbo ataka kurejeshwa kwa raia wa Côte d'Ivoire waliokimbilia Ghana

Rais  wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo alikuwa nchini Ghana kwa muda wa siku nne. Kwa mujibu wa taarifa ya chama chake, alienda nchini Ghana kushiriki mazishi ya Kapteni Kojo Tsikata, ambaye alikuwa afisa mwenye ushawishi na mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa Ghana, Jerry Rawlings.

Laurent Gbagbo, Juni 17, 2021.
Laurent Gbagbo, Juni 17, 2021. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Laurent Gbagbo pia aliwatembelea wakimbizi wa Côte d'Ivoire, ambao anataka warejee nchini. Baada ya kutimuliwa mamlakani kwa rais huyo wa zamani, raia 11,000 waCôte d'Ivoire walikimbia Ghana kufuati kuzuka kwa machafuko ya baada ya uchaguzi.

Damana Adia Pickass na Justin Koné Katinan, kiongozi wa zamani wa chama cha Ivorian Popular Front ni miongoni mwa watu maarufu zaidi na wanaomuunga mkono Gbagbo waliolazimika kutoroka nchi ya Côte d'Ivoire na kukimbilia Ghana - walirejea Côte d'Ivoire msimu wa masika uliopita. Lakini wafuasi wa Laurent Gbagbo bado ni wengi sana wanaoishi uhamishoni katika nchi hii jirani. "Takriban wafuasi 7,400" wako uhamishoni nchini Ghana, kulingana na chama cha PPA-CI, chama kipya cha Laurent Gbagbo.

Rais huyo wa zamani wa Côte d'Ivoire alikutana na wawakilishi wa wakimbizi hao mwishoni mwa juma hili lililopita mjini Accra. "Mkutano usio rasmi ambao haukupangwa katika programu," alisema Ousmane Sy Savané, meneja wa mawasiliano wa chama cha PPA-CI. Mkutano, hata hivyo, ni muhimu, lakini suala hili bado ni gumu, wamesema.

Maswali ya kiufundi na kifedha yanapaswa kutatuliwa

Kuanzia mwaka 2015, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi, UNHCR, lilisitisha kutoa huduma ya kifedha kwa raia hawa wa Côte d'Ivoire waliokuwa uhamishoni, maafisa wa zamani na wadau katika masuala ya kiuchumi, likiwatolea wito wa kurejea Côte d'Ivoire. Walikataa mara kwa mara, wakidai kuachiliwa kwa Laurent Gbagbo kama sharti.

Leo hali imebadilika. Kwa hivyo, kurudi kwa wakimbizi hawa kunawezekana. Laurent Gbagbo ameelezea matumaini yake kuwa watu hao wanaweza kurejea nchini. Masuala ya kifedha na vifaa bado yanasalia kutatuliwa. Baada ya zaidi ya miaka kumi uhamishoni, kurejeshwa nyumbani kunamaanisha gharama kubwa kwa familia hizi, ambazo zinabaini kwamba faranga za CFA 300,000 zinazotolewa na UNHCR hazitoshi kama fidia kwa wakimbizi. Wanaomba faranga milioni 2, lakini pia uwezekano wa kurejeshwa katika kwenye nafasi zao zao kazi serikalini.

Masuala haya yatashughulikiwa wakati wa mazungumzo ya kisiasa kati ya serikali na vyama vya upinzani ambayo yanatarajiwa kuanza tena rasmi Desemba 16, baada ya kukatizwa kwa zaidi ya miezi sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.