Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-HAKI

Serikali ya Côte d'Ivoire: Laurent Gbagbo bado anakabiliwa na mashitaka

Wakati wa mahojiano yake na France 24, rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo alirejea tena hukumu yake ya hadi kifungo cha miaka 20 iliyotolewa na jaji wa nchi hiyo katika kesi ya "kuvunjika kwa BCEAO", wakati alikuwa kizuizini katika Mahakama Kimataifa ya Uhalifu. Rais wa zamani ametupilia mbali kesi hiyo.

Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo, hapa ilikuwa Abidjan Julai 27, 2021.
Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo, hapa ilikuwa Abidjan Julai 27, 2021. REUTERS - LUC GNAGO
Matangazo ya kibiashara

Tangu arudi nchini Côte d'Ivoire amekuwa huru kutembea lakini bado hajapata msamaha kutoka kwa rais kwa kifungo aliohukumiwa. Siku ya Jumatano, Oktoba 20, serikali ilimjibu mkuu wa zamani wa nchi: bado anashtakiwa katika kesi hii.

Katika mahojiano marefu na France 24, Laurent Gbagbo alitoa tena wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kiraia na kijeshi, waliozuiliwa tangu mzozo wa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 na 2011 ambao ulisababisha vifo vya takriban watu 3,000. Suala la kuhukumiwa kwake mwenyewe, na mahakama ya Côte d'Ivoire, hadi kifungo cha miaka 20 jela katika kesi ya "kuvunjika kwa BCEAO" pia ilijadiliwa.

Tangu arudi Côte d'Ivoire mnamo Juni 17, Laurent Gbagbo hajawahi kuwa na wasiwasi na uamuzi huu wa mahakama, na alisema hasubiri msamaha wowote kutoka kwa rais ili kuondoa hukumu hii dhidi yake :

“Sijawahi kuiba benki. BCEAO imeibiwa na majambazi wengi, na waasi. Je! Ni Gbagbo ndiye anahukumiwa miaka 20? Hawatanifanya nikiri jambo lisilokubalika. "

"Bwana Gbagbo ana migogoro mingi ya kusuluhisha, ikiwa ni pamoja na masuala yanayomhusu"

Kwa kumjibu, msemaji wa serikali Amadou Coulibaly alisema Jumatano kwamba uamuzi huu uko halali licha ya ICC kuachiliwa Laurent Gbagbo kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu:

“Bwana Laurent Gbagbo ni kweli ashangae, bado anashitakiwa mbele ya mahakama ya Côte d'Ivoire. Sitaki kutoa maelezo zaidi kuhusiana na maneno ya Bw. Laurent Gbagbo, ambaye ana migogoro mingi ya kutatua, ikiwa ni pamoja na migogoro inaymhusu mwenyewe. "

Serikali hata hivyoinabaini kwamba rais Alassane Ouattara alikaribisha uwepo wa chama tawala wakati wa uzinduzi wa chama kipya cha Laurent Gbagbo, Oktoba 16-17. Hii inasaidia kuimarisha maridhiano ya kitaifa, kulingana na rais Ouattara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.