Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d’Ivoire: Laurent Gbagbo apendekeza kuundwa kwa chama kipya

Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire Laurent Ggagbo amependekeza, kwenye mkutano wa kamati kuu ya chama cha FPI, kuundwa kwa chama kipya cha kisiasa.

Rais wa zamani Laurent Gbagbo, hapa ilikuwa Abidjan Julai 27, 2021. Mwanzilishi wa chama cha FPI kilichohujumiwa na mgawanyiko, Laurent Gbagbo amependekeza kuundwa kwa chama kipya cha kisiasa.
Rais wa zamani Laurent Gbagbo, hapa ilikuwa Abidjan Julai 27, 2021. Mwanzilishi wa chama cha FPI kilichohujumiwa na mgawanyiko, Laurent Gbagbo amependekeza kuundwa kwa chama kipya cha kisiasa. REUTERS - LUC GNAGO
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani hataki kuingia katika vita vya kisheria na waziri wake mkuu wa zamani, Pascal Affi N’Guessan, ambaye anaongoza tawi moja la chama cha FPI, baada ya kugawanyika. Hivi ndivyo taarifa ya mwisho inavyoonyesha. Chama kipya, kulingana na vyanzo vya RFI, kinaweza kuundwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Laurent Gbagbo, kwa kuhalalisha pendekezo lake la kuunda chama kipya na "kumuachia Affi N'Guessan" jina hilo la FPI, amesema: "Unapotembea na kuona kikwazo njiani, lazima ukate kulia au kushoto au hata uruke. MMoja wa watu walioshiriki mkutano huo amekiri kuwa "hii itaturuhusu kufanya kazi kwa utulivu".

Kizuizi ambacho kiongozi Laurent Gbagbo, amezungumza kwa nusu saa, ni Affi N'Guessan, rais wa tawi la chama cha FPI kinachotambuliwa rasmi, bado anatuhumiwa kwa "kuteka chama."

Mgogoro huo ulianzia mwaka 2014. Upande wa chama cha Affi N’Guessan, wametangaza kwamba mkutano wa kamati kuu ya chama utafanyika Agosti 14.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.