Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d'Ivoire: Wafungwa 78 waachiliwa huru

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara ametangaza Ijumaa kuwaachiliwa huru watu 78 walioshikiliwa tangu mwaka 2020 kwa kupinga muhula wake wa tatu, ikiwa ni ishara mpya ya maridhiano ya kisiasa inayoonekana kwa miezi kadhaa nchini Côte d'Ivoire.

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara wakati wa hotuba yake kwa taifa Ijumaa, Agosti 6, 2021.
Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara wakati wa hotuba yake kwa taifa Ijumaa, Agosti 6, 2021. © Capture d'écran Facebook Live Présidence de la République de Côte d'Ivoire
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba alioitoa usiku wa kuamkia Siku ya Uhuru, rais Ouattara alitangaza "kuwekwa chini ya usimamizi wa mahakama au kuachiliwa kwa muda (...) watuhumiwa 69 waliowekwa kizuizini kufuatia matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba 2020" .

Aliongeza kuwa amewasamehe watu tisa waliopatikana na hatia ya makosa yaliyofanywa wakati wa matukio hayo. "Hali ya watu wengine wanaozuiliwa bado inachunguzwa," alisema.

Alassane Ouattara alichaguliwa tena mwezi Oktoba 2020 kwa muhula wa tatu uliozua utata katika uchaguzi wa urais uliosusiwa na upinzani ambao uliona kuwa muhula wa tatu wa Bw. Ouattara ni kinyume cha katiba, hali ambayo ilisababisha mzozo ambao uligharimu maisha ya karibu watu 100 na nusu elfu kujeruhiwa kati ya mwezi Agosti na Novemba 2020.

Mvutano huo umepungua na uchaguzi wa wabunge mwezi Machi ulifanyika kwa amani, na vyama vikuu vya upinzani vilishiriki katika uchaguzi huo na kukubali matokeo ya uchaguzi yalipelekea chama tawala kudhibiti vti vingi bungeni.

Hivi karibuni Laurent Gbagbo alikutana na rais Ouattara na kumuomba atazame jinsi ya kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa ambao wengi wao ni wafuasi kutoka chama cha Gbagbo.

Bw. Gbagbo alirejea nchini Côte d'Ivoiretarehe 17 Juni baada ya kuachiliwa na kufutiwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC mwishoni mwa mwezi Machi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.