Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-ICC

Côte d'Ivoire: ICC yafuta mashtaka dhidi ya Simone Gbagbo

Simone Gbabgo hakabiliwi tena na mashitaka kutoka Mahakama ya Kimlataifa ya Uhalifu, ICC. Waranti wa kukamatwa wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya mke wa rais wa zamani wa Côte d'Ivoire, aambaye alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa mzozo wa 2010-2011 yameondolewa.

Kiongozi wa chama cha FPI Simone Gbagbo, Agosti 11, 2020.
Kiongozi wa chama cha FPI Simone Gbagbo, Agosti 11, 2020. SIA KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mahakama inaamua kwamba hati ya kukamatwa dhidi ya Simone Gbagbo imefutwa na haina umuhimu tena,"imeandika ICC, ikijibu ombi kutoka kwa mwendesha mashtaka, katika uamuzi wa kurasa 7 wa Julai 19 na kutolewa hadharani Alhamisi jioni wiki hii.

Simone Gbagbo yuko huru kusafiri

"Habari njema kwa Bi Simone Gbagbo (...), sasa ataweza kusafiri akiwa uhuru kote ulimwenguni," amejibu wakili wake Ange Rodrigue Dadjé, katika taarifa.

"Kuondolewa kwa waranti huu kunakuja kumaliza kabisa kesi dhidi ya Simone Gbagbo mbele ya ICC," ameongeza.

Simone Gbagbo alikuwa ameshtakiwa na ICC tangu 2012 kwa makosa manne ya uhalifu dhidi ya binadamu, ambayo ni mauaji, ubakaji, vitendo vingine visivyo vya kibinadamu na mateso, yaliyofanywa wakati wa mzozo wa baada ya uchaguzi wa 2010-2011.

Mgogoro huu, uliozuka kufuatia hatu ya Laurent Gbagbo kukataa kutambua kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais wa 2010 dhidi ya Alassane Ouattara, ulisababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000.

Simone Gbagbo ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Mwezi Machi mwaka jana, ICC ilimuachilia huru Laurent Gbagbo, ambaye pia alishtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, na aliweza kurudi Côte d'Ivoire Juni 17, baada ya miaka kumi akizuiliwa Hague.

Tofauti na mumewe, Simone Gbagbo alikuwa hajawahi kukabidhiwa ICC.

Hata hivyo alihukumiwa mwezi Machi 2015 kwa miaka 20 gerezani huko Abidjan kwa kuhatarisha usalama wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.