Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d’Ivoire: Gbagbo bega kwa bega na wafungwa wa kisiasa

Siku chache baada ya kurejea nchini Côte d’Ivoire na siku chache baada ya kukutana kwa mazungumzo na rais Alassane Ouattara, rais wa zamani Laurent Gbagbo, Jumatatu, Agosti 2, alikutana na mashirika kadhaa ya wake wa wanaharakati wa kisiasa wanazuiliwa jela kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2010-2011 na yale ya mwaka 2020. Laurent Gbagbo alisema atafanya kila aliwezalo ili  wafungwa hawa waweze kuachiliwa huru.

Laurent Gbagbo, Juni 28, 2021.
Laurent Gbagbo, Juni 28, 2021. © AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

"Ni mapambano yangu", alisema Laurent Gbagbo mbele ya wanawake zaidi ya mia moja, waliokusanyika mjini Abidjan. Julai 27, rais wa zamani alimkabidhi Alassane Ouattara orodha ya majina 110 ya wafungwa. Kuhusu kuachiliwa kwao, Laurent Gbagbo alihakikisha kuwa rais wa sasa "hakumwambia hapana, na wala hakusema ndiyo" pia, akimaanisha kuwa Ouattara alimthibitishia "kufanya kila aliwezalo ili wafungwa hao waweze kuachiliwa huru haraka iwezekanavyo".

Orodha ya wafungwa hawa 110 ni pamoja na watu waliokamatwa baada ya mzozo wa 2010-2011, watu waliokamatwa mwaka 2020 wakati wa kampeni ya uchaguzi wa urais lakini pia wale waliokamatwa mwezi Juni kando ya kurejea kwa Laurent Gbagbo nchini Côte d'Ivoire. Ingawa kulingana na orodha hiyo, anabaini kwamba wafungwa wote ni wa kisiasa, baadhi yao walihukumiwa kwa uhalifu wa kumwaga damu, kama Jenerali Brunot Dogbo Blé.

Kulingana na vyombo vya habari nchini Côte d'Ivoire, Laurent Gbagbo pia alitaja, "kwa maneno mawili" kesi ya Guillaume Soro na watu walio uhamishoni wanaopinga utawala wa Alassane Ouattara. Mbele ya wake za wafungwa na hasa chama cha GPS, chama cha Guillaume Soro, Laurent Gbagbo alihakikishia umati kwamba "pia atapaza sauti", ili watu hao "waweze kurejea nchini".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.