Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d'Ivoire: Alassane Ouattara na Laurent Gbagbo wakutana kwa mlara ya kwanza

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara alimpokea mtangulizi wake Laurent Gbagbo Jumanne wiki hii, mkutano ambao unaelezwa kuwa wa kihistoria katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko ya baaada ya uchaguzi katika miaka ya 2010-2011. Mkutano huo ulifanyika katika ikulu ya rais huko Abijan na ulidumu saa moja.

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara alimkaribisha mtangulizi wake Laurent Gbagbo katika ikulu ya rais huko Abidjan Julai 27, 2021, wakati wa mkutano wao wa kwanza tangu mzozo wa baada ya uchaguzi wa 2010-11.
Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara alimkaribisha mtangulizi wake Laurent Gbagbo katika ikulu ya rais huko Abidjan Julai 27, 2021, wakati wa mkutano wao wa kwanza tangu mzozo wa baada ya uchaguzi wa 2010-11. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Baada ya saa moja ya mazungumzo, Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara walifanya mkutano na vyombo vya habari na kila mmoja kuelezea hisia zake baada ya mkutano wao.

Marais hao wawili kila mmoja alitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika mazingira mazuri ya kirafiki na ya kindugu.

Kwanza Laurent Gbagbo alibaini kwamba wakati wa mazungumzo na rais Alassane Ouattara alizungumzia suala la wafungwa wa kisiasa waliowekwa kizuizini tangu mgogoro mbaya uliyoibuka baada ya uchaguzi wa 2010-2011, ambao umekuwa chanzo cha mvutano kwa kambi hizo mbili miaka kumi sasa. Laurent Gbagbo ameomba wafungwa hao waachiliwe huru, huku akimuachia kazi hiyo rais Alassane Ouattara kama jaji pekee ambaye ana maamuzi ya mwisho.

Mikutano mingine yatarajiwa kufanyika katika siku zijazo

Rais Alassane Ouattara, ambaye kwanza alianza kwa kumshukuru Laurent Gbagbo, pia kutoa rambirambi zake kwa Laurent Gbagbo juu ya kifo cha mama yake, ambaye alifariki dunia wakati akiwa kizuizini ICC. "Hali hiyo inakumbusha kifo cha mama yangu aliye wakati nikiwa uhamishoni nchini Ufaransa katikati ya miaka ya 2000, na Laurent Gbagbo, wakati huo rais, alinisaidia kurudi nchini kumzika mama yangu", amesema Bw. Ouattara.

Alassane Ouattara pia alikaribisha mkutano huu wa kwanza: "Mkutano huu ulikuwa muhimu kurejesha uaminifu kati ya yetu," alisema. Alihakikisha kuwa mikutano mingine na mtangulizi wake itafanyika katika siku za usoni, baada ya mwezi Agosti kulingana na rais. Wanasiasa wenine watashirikiswa katika mikutano hiyo, ameongeza rais Alassane Ouattara.

Wote wawili Rrais alassane Ouattara na Laurent Gbagbo walisisitiza utayari wao wa kusonga mbele. Na kabla ya yote, ni kuelekea maridhiano ya kweli ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.