Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIMONE GBAGBO

Simone Gbagbo avunja ukimya baada ya kurejea nyumbani kwa mumewe

Kwa mara ya kwanza tangu mumewe arudi nchini Cote d'Ivoire Juni 17, mke wa rais wa zamani Laurent Gbagbo  amejitokeza kupitia ujumbe uliochapishwa kwenye mitandao yake ya kijamii.

Simone Gbagbo mke wa rais wa zamani wa Cote Dvoire,  14 Septemba  2019
Simone Gbagbo mke wa rais wa zamani wa Cote Dvoire, 14 Septemba 2019 © AFP - Sia Kambou
Matangazo ya kibiashara

Simone Gbagbo amekaribisha hatua ya kurejea kwa mumewe nchini, lakini ameomba hatua zaidi zitekelezwe ili kupata maridhiano ya kudumu.

Hata hivyo Simone hakuzungumzia lolote kuhusu kesi ya talaka iliowasilishwa na Gbagbo siku chache baada ya kurejea nchini.

Kurejea huku ilikuwa pia matokeo ya makubaliano na rais Allasane Ouattara kumuona rais Laurent Gbagbo akirejea nchini mwake, namwambia asante sana kwa hilo. Najitokeza pia kumuomba kuendelea kutekeleza vitendo vikubwa vya utulivu na maridhiano ambavyo wananchi wengi wa Cote d’Ivoire wanatarajia.

 

 

Hususan kumrejesha nyumbani Charles Blegude na wananchi wote wa cote d’Ivoire ambao bado wapo uhamishoni. Kuwaacha huru wafungwa wote wa kisiasa na wanajeshi wa mzozo wa baada ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.