Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d'Ivoire: Laurent Gbagbo kukutana na Alassane Ouattara katika ikulu ya rais

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara na mtangulizi wake Laurent Gbagbo wanatarajiwa kukutana Jumannehii Julai 27, mkutano wa kwanza tangu uchaguzi wa urais wa 2010 ambao ulisababisha machafuko makubwa.

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (kuliaa) na mtangulizi wake Laurent Gbagbo (kushoto).
Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (kuliaa) na mtangulizi wake Laurent Gbagbo (kushoto). ISSOUF SANOGO, KAMBOU SIA AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu kiongozi wa zamani wa nchi hiyo kurejea nchini mwezi uliopita baada ya kuachiliwa huru katika mahakama ya ICC, wengi wameendelea kusubiri mkutano huo wa kwanza kati ya wawili hao, mkutano ambao unatarajia kuashiria hatua muhimu kuelekea maridhiano ya kitaifa na kuboresha hali ya kisiasa.

Jumanne Julai 27 utafanyika mkutano wa kwanza kati ya Alassane Ouattara na Laurent Gbagbo tangu machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2010-2011, ambao ulisababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000 nchini Côte d'Ivoire kulingana na Umoja wa Mataifa. Itakuwa pia tarehe yao ya kwanza kukutana tangu kurudi kwa mpinzani huyo wa kihistoria mwezi uliopita.

Wiki iliyopita msemaji wa serikali Amadou Coulibaly, alihakikisha kwamba rais anajaribu kukutana na wapinzani wake. "Kuna mazungumzo ambayo yalianza na Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly, ambayo yaliendelea na Waziri Mkuu Hamed Bakayoko na Waziri Mkuu Achi," amesema.

Mnakumbuka mikutano yote hapo ilikuwa ya kujiandaa kurudi kwa Laurent Gbagbo. Hakujawahi kuwa na usumbufu wowote katika mazungumzo katika nchi yetu na yataendelea kwa sababu hii ni nia njema ya serikali.

Msemaji wa serikali ya Cote d'Ivoire alitangaza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Abidjan Jumatano wiki iliyopita. Amadou Coulibaly alitangaza kuwa rais Alassane Ouattara atampokea Laurent Gbagbo Julai 27, Jumanne ya wiki ijayo, katika ikulu ya rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.