Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d'Ivoire: Wafuasi wa Laurent Gbagbo sasa wasubiri chama kipya

Wafuasi wa rais wa zamaniwa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo wanaendelea kusubiri kutangazwa kwa chama kipya siku chache baada ya kiongozi wao kuamua kuachana na chama cha FPI, chama alichounda mafichoni mnamo mwaka 1982.

Laurent Gbagbo huko Abidjan. Wafuasi, walioshikamana sana na FPI, wana uchungu, lakini wanaamua kumfuata kiongozi wao.
Laurent Gbagbo huko Abidjan. Wafuasi, walioshikamana sana na FPI, wana uchungu, lakini wanaamua kumfuata kiongozi wao. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Katika "vita" vya kudhibiti chama na Pascal Affi N'Guessan, mahakama iliidhinisha waziri mkuu wake wa zamani kuchukuwa chama. Siku ya Jumatatu wiki hii Bw. Gbagbo alisema anasitisha kushiriki katika vita vya kisheria visivyo na mwisho na ameamua kuunda chama kipya.

Wanaharakati wake, walioshikamana sana na chama cha FPI, walipata taarifa hiyo baada ya kikao cha kamati kuu ya chama.Licha ya kughadhabishwa na hatua hiyo, wanaamua kumfuata kiongozi wao.

FPI ni moja ya vyama vya zamani zaidi nchini Cote d'Ivoire, kikiwa na karibu miaka 40 tangu kuanzishwa kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.