Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Côte d'Ivoire: Wafuasi thelathini wa upinzani wahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela

Wafuasi 30 kutoka chama cha upinzani cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo walihukumiwa Alhamisi jioni kifungo cha miaka miwili jela kwa "kuhatarisha usalama wa umma", wakati wa maandamano mwishoni mwa mwezi Februari huko Abidjan.

Rais wa zamani waCôte d'Ivoire Laurent Gbagbo, kiongozi wa sasa wa African Peoples' Party - Côte d'Ivoire (PPA-CI), mnamo Oktoba 17, 2021, mjini Abidjan.
Rais wa zamani waCôte d'Ivoire Laurent Gbagbo, kiongozi wa sasa wa African Peoples' Party - Côte d'Ivoire (PPA-CI), mnamo Oktoba 17, 2021, mjini Abidjan. © AP - Diomande Ble Blonde
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Februari 24, watu 31 walikamatwa na kuwekwa kizuizini wakati wakiandamana uungaji wao mkono kwa katibu mkuu wa Chama cha African Peoples' Party - Côte d'Ivoire (PPA-CI), Damana Pickass, ambaye aliitwa na jaji mchunguzi kwa jukumu lake katika shambulio la kambi moja mjini Abidjan mnamo mwaka 2021.

Ishirini na saba kati ya waandamanaji hawa walifikishwa mahakamani Alhamisi jioni na wote isipokuwa mmoja - aliyeachiliwa - walihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela. Upande wa mashtaka uliomba kifungo cha miaka mitatu.

Wakati wa kesi hiyo ikisikilizwa, mmoja wa waendesha mashtaka alibaini kuwa washtakiwa wamepatikana na hatia ya kuhatarisha usalama wa umma, "hata bila vurugu". Alikumbusha kwamba wito wa Bw. Pickass ulikuwa wa "binafsi" na kwamba haukupaswa kusababisha mkutano wa hadhara.

"Ushahidi haujatolewa. Dhana iliyofafanuliwa ya kuhatarisha usalama wa umma ni aina ya kuwakamata wote", alilaumu wakili wa utetezi, Me Jonas Zadi, akibainisha kwamba atakata rufaa dhidi ya hukumu hii. "Watu ambao wamehukumiwa wote ni wafuasi wa chama cha PPA-CI, ni kitendo," aliongeza wakili mwingine wa upande wa utetezi, Wakili Sylvain Tapi.

Wiki iliyopita, msemaji wa PPA-CI, Justin Koné Katinan alishutumu utawala kuvishawishi vyombo vya sheria "kwa madhumuni ya kisiasa", baada ya kukamatwa watu hao. "Mahakama imekuwa chombo cha kuwakandamiza wapinzani wa utawala," alisema.

"Utawala wetu, unajaribu kujumuisha utawala wa sheria ambapo kila raia yuko huru kutumia uhuru wake kwa mujibu wa sheria zinazotumika," amesema Mamadou Touré, naibu msemaji wa chama tawala cha RHDP.

Hali ya kisiasa hata hivyo imedorora tangu uchaguzi wa urais wa 2020, wakati Alassane Ouattara alipochaguliwa tena kwa muhula wa tatu wenye utata, ambapo ghasia zilisababisha vifo vya watu 85 na 500 kujeruhiwa.

Uchaguzi wa wabunge ulifanyika kwa utulivu Machi 2021, na wanasiasa wa upinzani Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé walirejea nchini, baada ya kuachiliwa na Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.