Pata taarifa kuu
USALAMA BARABARANI

Kumi na tano waangamia katika ajali ya magari mawili yaliogongana Côte d'Ivoire

Watu 15 walifariki Jumamosi katika ajali ya barabarani baada ya basi ndogo kugongana na lori katikati mwa Côte d'Ivoire, Waziri wa Uchukuzi Amadou Koné ametangaza hivi punde.

Magari yalikwama katika msongamano wa magari katika wilaya ya Plateau huko Abidjan, Côte d'Ivoire, Desemba 19, 2019.
Magari yalikwama katika msongamano wa magari katika wilaya ya Plateau huko Abidjan, Côte d'Ivoire, Desemba 19, 2019. © Ludovic Marin / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kati ya watu 1,000 na 1,500 wanauawa kila mwaka katika ajali za barabara nchini Côte d'Ivoire, kulingana na Wizara ya Uchukuzi.

"Jumamosi, karibu saa moja usiku., ajali mbaya ya barabarani ilitokea kwenye barabara inayounganisha miji ya Katiola na Bouake," waziri amesema katika taarifa.

"Ajali hiyo iliyogharimu maisha ya watu 15 na wengine kadhaa kujeruhiwa, imeiweka nchi yetu katika mswiba mwingine, baada ya gari dogo kugongana na lori la kusafirisha mizigo lililoegeshwa", amengeza.

Ajali mbaya hutokea mara kwa mara nchini Côte d'Ivoire, kutokana na ubovu wa baadhi ya barabara na magari mengi, pamoja na utovu wa nidhamu wa madereva.

Madereva wengi pia ni wamiliki wa vibali vilivyonunuliwa, bila khata hivyo kupitia shule ya udereva.

Côte d'Ivoire ilianzisha leseni iliyojaza alama mnamo Machi 1. Kila dereva aliye na leseni ana alama 12 ambazo zinaweza kuondolewa hatua kwa hatua kulingana na makosa anayoyafanya kwa uendeshaji wake mbovu.

Kati ya watu 1,000 na 1,500 wanafariki kila mwaka katika ajali za barabara nchini Côte d'Ivoire, kulingana na Wizara ya Uchukuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.