Pata taarifa kuu

Côte d'Ivoire: Gazeti la kila siku la upinzani lasimamishwa kwa "kudhoofisha" shughuli za mahakama

Gazeti la kila siku la upinzai nchini Côte d'Ivoire limesimamishwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Vyombo vya Habari (ANP), chombo kinacosimamia vyombo vya habari nchini Côte d'Ivoire, ambacho kinalishutumu kwa 'kuidhoofisha' 'shughuli za mahakama'.

 ANP imetangaza kusimamishwa kwa matoleo sita ya Gazeti la kila siku la Le Temps, linalounga mkono rais wa zamani Laurent Gbagbo na kumuwekea marufuku mhariri wake, Yacouba Gbane, kuandika kwa kipindi cha miezi mitatu.
ANP imetangaza kusimamishwa kwa matoleo sita ya Gazeti la kila siku la Le Temps, linalounga mkono rais wa zamani Laurent Gbagbo na kumuwekea marufuku mhariri wake, Yacouba Gbane, kuandika kwa kipindi cha miezi mitatu. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa siku ya Jumatano, ANP imetangaza kusimamishwa kwa matoleo sita ya Gazeti la kila siku la Le Temps, linalounga mkono rais wa zamani Laurent Gbagbo na kumuwekea marufuku mhariri wake, Yacouba Gbane, kuandika kwa kipindi cha miezi mitatu.

ANP inalikosoa gazeti hilo hasa kwa kuchapisha picha ya hakimu anayechunguza kesi, ambayo "inakiuka haki zake za picha na kudhoofisha shughuli zake, usiri wa uchunguzi" na "kuhatarisha usalama wake".

Hakimu alimuitisha mara mbili Damana Pickass, katibu mkuu wa chama cha African Peoples' Party Côte d'Ivoire (PPA-CI) kilichoundwa na Laurent Gbagbo. Alisikilizwa kwa madai ya jukumu lake katika shambulio la kambi ya jeshi huko Abidjan mnamo 2021.

ANP inanyooshea kidole makala ya pili pia iliyoandikwa na Yacouba Gbane, kuhusu kesi hiyo, ambapo mwandishi wa habari anawashutumu "majaji" kwa "kuwa silaha zisizo halali za utawala" wa Rais Alassane Ouattara.

Kifungu hicho kinarejelea kifungo cha miaka miwili jela kwa "kuvuruga utulivu wa umma", mnamo Machi 9, kati ya wanaharakati 26 wa PPA-CI ambao walikuja kumuunga mkono Bw. Pickass wakati akiitishwa kwa mara ya kwanza: walihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.