Pata taarifa kuu

Msumbiji yahalalisha wanamgambo wa ndani kupigana na wanajihadi

Mamlaka nchini Msumbiji imehalalisha kuwepo kwa wanamgambo wa ndani ili kupigana na waasi wa kijihadi kaskazini mashariki mwa nchi. Kwa miaka 5, jimbo la Cabo Delgado limekuwa likikumbwa na waasi wa kijihadi, ambao wanajiita ndani ya nchi "Al Shabab". 

Kwa miaka 5, jimbo la Cabo Delgado limekuwa likikumbwa na waasi wa kijihadi.
Kwa miaka 5, jimbo la Cabo Delgado limekuwa likikumbwa na waasi wa kijihadi. AFP - CAMILLE LAFFONT
Matangazo ya kibiashara

Licha ya usaidizi wa wanajeshi wa kikanda, mzozo huo umekwama. Wiki iliyopita, serikali ilipitisha amri ya kutambua na kuidhinisha wanamgambo hawa, waliopewa jina la "Forca Local", kufanya kazi pamoja na vikosi vya jeshi vilivyopo katika jimbo hili.

Wanamgambo hawa wanakadiriwa kuwa mia kadhaa, wanaoundwa hasa na maveterani wa mapambano ya uhuru, kutoka kabila la bara katika jimbo la Cabo Delgado. Wakiwa wanadhaminiwa na serikali, wanamgambo hawa, waliopewa jina la "Forca Local", wamekuwa wakipigana dhidi ya makundi ya Kiislamu kwa miaka kadhaa, lakini hadi sasa walikuwa hawajatambuliwa kisheria.

Kwa hiyo amri hii inawafanya kutambuliwa rasmi. Hili ni jambo la ziada kukiri kwamba wanajeshi wa kawaida waliopo nchini Msulbiji hawawezi kuangamiza waasi wa Kiislamu, anabaini mtafiti mmoja. Jeshi la Msumbiji linaungwa mkono na wanajeshi wa Rwanda, pamoja na wanajeshi kutoka SADC, Jumuiya ya kikanda, ambao wote kwa ujumla ni zaidi ya wanajeshi 6,000.

Mashirika kadhaa ya kiraia yanashutumu kuongezeka kwa wanajeshi nchini humo pamoja na ongezeko la matumizi ya kijeshi kama suluhisho pekee la mgogoro huo.

Kwa mtafiti Borges Nhamirre, wa Taasisi ya Mafunzo ya Usalama, anasema hata ikiwa ni bora kwa wanamgambo hao kupigana ndani ya mfumo wa kisheria, matumizi yao sio suluhisho la kupigana na wanajihadi. Ni bora kuwa na jeshi ambalo lina vifaa bora na mafunzo bora, hasa katika suala la kuheshimu haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.