Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu 190 wameripotiwa kufariki katika kimbunga Freddy nchini Malawi

NAIROBI – Nchini Malawi, kimbunga Freddy ambacho kimeambatana na mafuriko makubwa kimesababisha vifo vya watu 190 kufikia Jumanne usiku.

Raia nchini Malawi wakiwatafuta wapendwa wao waliouawa katika Kimbunga Freddy
Raia nchini Malawi wakiwatafuta wapendwa wao waliouawa katika Kimbunga Freddy REUTERS - ELDSON CHAGARA
Matangazo ya kibiashara

Hali inaripotiwa kuwa mbaya katika jiji la Kibiashara la Blantyre, ambako mbali na vifo watu wamepoteza makaazi yao na kuharibika kwa miundo mbinu kama barabara.

Penjani Sowoya ni mkaazi wa jiji hilo anayefanyakazi na Shirika la Malawi Land Rover Defender Club linalowasaidia watu waliothirika na kimbunga hiki.

“Makaazi ya watu yameharibiwa sana ambapo tumekuwa tukitumia njia ambazo zinapitika kama njia moja ya kuwafikia watu walioathirika na hali hii.”amesema Penjani Sowoya.

Takriban watu 20,000 nchini humo wameathiriwa na hali mbaya ya hewa, kulingana na Umoja wa Mataifa. Kimbunga hicho kilitokea katika nchi jirani ya Msumbuji.

Mashirika ya misaada ikiwemo lile la msalaba mwekundu yanaedelea na juhudi za kuwasiaidia raia walioathirika na kimbunga hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.