Pata taarifa kuu

Msumbiji: janga mbaya zaidi la kipindupindu katika zaidi ya muongo mmoja kulingana na WHO

Msumbiji inakabiliwa na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu kuwahi kutokea katika zaidi ya muongo mmoja kufuatia kimbunga Freddy, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharuisha siku ya Ijumaa.

Kufikia sasa, wilaya 47 katika majimbo manane kati ya 11 ya nchi hiyo zimeathirika, kulingana na WHO. Kampeni ya kwanza ya chanjo dhidi ya kipindupindu ilifanyika mwishoni mwa mwezi Februari katika mikoa minne, ikilenga zaidi ya watu 715,000. Kampeni ya pili ilizinduliwa Alhamisi huko Quelimane, ikilenga watu 410,000. Wengine watafuata, hasa katika majimbo ya Manica na Sofala.
Kufikia sasa, wilaya 47 katika majimbo manane kati ya 11 ya nchi hiyo zimeathirika, kulingana na WHO. Kampeni ya kwanza ya chanjo dhidi ya kipindupindu ilifanyika mwishoni mwa mwezi Februari katika mikoa minne, ikilenga zaidi ya watu 715,000. Kampeni ya pili ilizinduliwa Alhamisi huko Quelimane, ikilenga watu 410,000. Wengine watafuata, hasa katika majimbo ya Manica na Sofala. LUSA - ANDRÉ CATUEIRA
Matangazo ya kibiashara

"Mlipuko wa kipindupindu hutokea mara kwa mara nchini Msumbiji kati ya mezi Oktoba na Aprili, lakini kwa karibu wagonjwa 21,000 na vifo 95, huu ni mlipuko mkubwa zaidi katika zaidi ya muongo mmoja," mwakilishi wa WHO nchini Msumbiji, Dk Severin Ritter von Xylander almewaambia waandishi wa habari huko Geneva, katika mkutano wa video kutoka Maputo.

Kwa mfano, jimbo la Manica (katikati-mashariki), ambalo sasa limeathiriwa kwa kiasi kikubwa, halijakumbwa na kipindupindu kwa muda wa miaka 15 iliyopita.” Afisa huyo wa WHO ameonya kwamba "mlipuko huo unaendelea kuenea katika maeneo mbalimbali", akibaini kwamba wilaya tano mpyaziliathirika katika wiki iliyopita pekee.

Katika mji wa bandari ulioathirika zaidi wa Quelimane, ambao umekosa maji wala umeme kwa siku 14, watu 132 wamelazwa katika vituo vya matibabu ya kipindupindu katika muda wa saa 24 zilizopita, amesema kwa mfano, akibaini kwamba "idadi ya wagonjwa zimeongezeka" na kuzidishwa na kumi.

Kufikia sasa, wilaya 47 katika majimbo manane kati ya 11 ya nchi hiyo zimeathirika, kulingana na WHO. Kampeni ya kwanza ya chanjo dhidi ya kipindupindu ilifanyika mwishoni mwa mwezi Februari katika mikoa minne, ikilenga zaidi ya watu 715,000. Kampeni ya pili ilizinduliwa Alhamisi huko Quelimane, ikilenga watu 410,000. Wengine watafuata, hasa katika majimbo ya Manica na Sofala.

Kwa jumla, zaidi ya watu milioni 1.35 wanalengwa na kampeni hizi. Mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga hicho "yanapungua sasa, lakini upatikanaji wa maji ya kunywa na usafi wa mazingira bado ni mgumu, karibu theluthi moja ya mazao yameharibiwa," ameongeza Dk Ritter von Xylander.

Kimbunga Freddy kilipiga eneo la Kusini mwa Afrika mara mbili katika muda wa wiki kadhaa. Nchini Msumbiji, iliharibu zaidi ya nyumba 132,000 na watu 184,000 walilazimika kuyahama makazi yao, kulingana na WHO. Na vituo vya afya 163 viliharibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.