Pata taarifa kuu

Msumbiji na Malawi zakumbwa na kimbunga Freddy

NAIROBI – Msumbiji na Malawi zimepata pigo kubwa baada ya kukumbwa na Kimbunga cha KiTropiki Freddy, ambacho kiliua zaidi ya watu 100, kujeruhi watu wengi na kusababisha uharibifu mkubwa wakati kilipokumba kusini mwa Afrika kwa mara ya pili katika mwezi mmoja mwishoni mwa juma.

Nchi za Msumbiji na Malawi zakabiliwa na kimbunga Freddy
Nchi za Msumbiji na Malawi zakabiliwa na kimbunga Freddy LUSA - ANDRÉ CATUEIRA
Matangazo ya kibiashara

Freddy ni mojawapo ya dhoruba kali zaidi kuwahi kurekodiwa katika ulimwengu wa kusini na inaweza kuwa kimbunga cha muda mrefu zaidi cha kitropiki, kulingana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani.

Kimbunga hicho kilikumba eneo la kati la Msumbiji siku ya Jumamosi, na kuezua paa za majengo na kuleta mafuriko kuzunguka bandari ya Quelimane, kabla ya kuelekea Malawi na mvua kubwa iliyosababisha maporomoko ya ardhi.

Kiwango kamili cha uharibifu na vifo nchini Msumbiji bado hakijabainika, kwani umeme na mawimbi ya simu yalikatika katika baadhi ya maeneo ya eneo lililoathiriwa.

Dhoruba hiyo imeua watu 99 nchini Malawi, wakiwemo 85 katika kitovu kikuu cha kibiashara cha Blantyre, alisema Charles Kalemba, kamishna wa idara ya maswala ya usimamizi wa majanga, siku ya Jumatatu.

Jumla ya waliouawa na kimbunga Freddy huko Msumbiji, Malawi na Madagascar tangu ilipotua kwa mara ya kwanza mwezi uliopita sasa ni takriban 136.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.