Pata taarifa kuu

Ghana yatumbukia katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi

Mfumuko wa bei wa zaidi ya 50%, kuporomoka kwa sarafu, kupanda maradufu kwa bei kwenye vituo vya mafuta... Ghana kwa sasa inapitia mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

Siku ya Jumanne serikali ilitia saini mkataba wa kunusuru dola bilioni 3 na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF katika jitihada za kuimarisha fedha zake za umma, lakini utulivu wa kiuchumi bado uko mbali.
Siku ya Jumanne serikali ilitia saini mkataba wa kunusuru dola bilioni 3 na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF katika jitihada za kuimarisha fedha zake za umma, lakini utulivu wa kiuchumi bado uko mbali. © WikimediaCommons CC CIAT
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na mfumuko wa bei wa kihistoria wa zaidi ya 50%, kuporomoka kwa kiwango cha fedha za ndani kwa 50%, bei kwenye vituo vya mafuta ambayo imeongezeka maradufu na deni ambalo ulipaji wake unameza nusu ya mapato ya serikali, Ghana inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Ni mgogoro mbaya zaidi katika miongo kadhaa.

Siku ya Jumanne serikali ilitia saini mkataba wa kunusuru dola bilioni 3 na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF katika jitihada za kuimarisha fedha zake za umma, lakini utulivu wa kiuchumi bado uko mbali.

Hadi miaka michache iliyopita, Ghana ilikuwa kielelezo cha utulivu wa kiuchumi na kisiasa katika eneo la Afrika Magharibi lililokumbwa na mapinduzi na ghasia za makundi ya kijihadi. Lakini kama sehemu kubwa ya bara, nchi ilijitahidi kupata nafuu kutokana na mdororo uliosababishwa na janga Uviko, kabla ya kupigwa ghafla na kuzorota kwa uchumi kutoka kwa vita vya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.