Pata taarifa kuu

Wafanyabiashara wa Ghana wafunga maduka kutokana na mfumko wa bei uliokithiri

Wafanyabiashara mjini Accra, mji mkuu wa Ghana, wameamua kufunga maduka siku ya Jumatano kama sehemu ya maandamano ya siku tatu ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha ambayo imekuwa mbaya zaidi tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kulingana na chama cha Wafanyabiashara nchini Ghana, kufungwa kwa biashara ni wito wa msaada kutoka kwa serikali.
Kulingana na chama cha Wafanyabiashara nchini Ghana, kufungwa kwa biashara ni wito wa msaada kutoka kwa serikali. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Shughuli zimezorota katika eneo la kibiashara na sehemu kunakouzwa bidhaa za magari,kutokana na msongamano wa magari.  Wachuuzi wa chakula pekee ndio walikuwa wakionekana mbele ya biashara zilizofungwa. Kwa kulemewa na madeni makubwa, Ghana ilirekodi mfumuko wa bei wa kihistoria wa 37% mwezi Septemba, wakati sarafu yake - cedi - ilishuka dhidi ya dola ya Marekani.

Rais Nana Akufo-Addo anakosolewa kwa usimamizi wake wa uchumi wa nchi hiyo na hasa kwa kuanzisha majadiliano na Shirika la Fedha la Kimataifa,-IMF - ambayo aliwahi kuahidi "Ghana bila msaada" - kupata mkopo wa dola bilioni tatu. Uamuzi huu ulizua hofu kwamba serikali ingeweka hatua za kubana matumizi ambazo zingezidi kuwaelemea watu, ambao tayari wanakabiliwa na mlipuko wa bei.

Kwesi Amoah, mfanyabiashara wa vipuri vya gari huko Abossey Okai, viungani mwa Accra, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wafanyabiashara walikuwa hawatoi tena bili, huku bei ikipanda haraka, wakati mwingine kwa muda wa saa chache. "Tunaelewa kuwa nyakati ni ngumu duniani kote, lakini majirani zetu nchini Côte d'Ivoire na Burkina Faso hawateseke kama sisi," amelaumu.

Muungano wa Wafanyabiashara wa Ghana (Guta) umesema kufungwa kwa maduka ni ombi la usaidizi kutoka kwa serikali na njia ya kudhihirisha kufadhaika kwao. "Ni dhahiri kwamba hatuwezi kustahimili (hali hii) tena," mwenyekiti wa Guta Joseph Obeng almesema.

Baraza la Serikali, chombo cha ushauri kilichoidhinishwa kikatiba na rais, kimejaribu kuwashawishi wenye maduka kusitisha mgomo huo, bila mafanikio. Serikali haikutoa maoni yoyote.

"Bwana Akufo-Addo anatukatisha tamaa. Tulipiga kura ya mabadiliko na njia bora ya maisha," amesema Doris Andoh, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 37. "Nina watoto wanne, na hivi tunavyozungumza, wawili wako nyumbani kwa sababu siwezi kuwalipia ada ya shule."

Benki kuu ya Ghana imepandisha kiwango chake kikuu cha sera kwa asilimia 10 mwaka huu hadi 24.5% katika jaribio la kudhibiti ukuaji wa bei. Lakini imeongeza gharama za kukopa kwa wafanyabiashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.