Pata taarifa kuu
GHANA- AFYA

Ghana imedhibitsiha kisa cha kwanza cha kirusi hatari cha Marburg

Watu wawili wa familia moja wamedhitishwa kuambukizwa virusi hatari vya Marburg nchini Ghana, virusi vinavyosemekana kusababisha Ebola.

Picha inayonyesha  virus Marburg vilivyoripotiwa  nchini Ghana.
Picha inayonyesha virus Marburg vilivyoripotiwa nchini Ghana. © CDC/ Dr. Frederick Murphy
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini humo inasema wawili hao walifariki wakati wakipokea matibabu kusini mwa eneo la Ashanti.

Watu 98 wameekwa karatanini katika taifa hilo la Afrika magharibi baada yao kushukiwa kutangamana na watu waliokuwa wameambukizwa.

Shirika la afya duniani (WHO), limeisifia Ghana kwa namna ambavyo imelishugulikia swala hilo kwa haraka.

Mkuu wa WHO katika ukanda wa Afrika Dr Matshidiso Moeti, anasema Marburg inaweza ikawa hatari zaidi iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kwa wakati.

Hadi sasa, matibau ya Marburg hayajapatikana japokuwa madaktari wanasema kunywa maji mengi pamoja na kutafuta huduma za wahudumu wa afya kwa haraka inamchango mkubwa katika kupamabana na virusi hivyo.

Marburg inasambazwa kwa binadamu kutoka kwa popo matunda ambapo inasambaa kwa binadamu kupitia maji maji ya mwili.

Hii ni mara ya pili kwa Marburg kupatikana Afrika magharibi.Kisa cha kwanza kilipatikana nchini Guinea mwaka jana japokuwa mlipuko huo ulitangazwa rasimi majuma matano baadae.

WHO inasema kuwa Marburg pia imewahi kudhibitishwa katika mataifa mengine ya Afrika ikiwemo Angola, DRC, Kenya, Afrika kusini na Uganda.  

Watu zaidi ya 200 walifariki kutokana na maambukizi ya virusi hivyo nchini Angola mwaka wa 2005. Hali iliyotajwa na WHO kuwa mbaya zaidi kuwahi tokea katika ukanda wa Afrika.

Kisa cha kwanza cha Marburg kilitangazwa nchini Ujerumani mwaka wa 1967 ambapo watu 7 walifariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.