Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mapigano makali yaripotiwa kati ya makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali

Mapigano kati ya makundi yenye silaha katika siku za hivi karibuni yamesababisha vifo vya watu kadhaa kaskazini mwa Mali, katika mikoa ya Ménaka na Gao, inayokumbwa na ghasia za wanajihadi, kulingana na maafisa wa kijeshi na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka mashirika ya propaganda ya wanajihadi.

Wanajeshi wakipata mafunzo katika kambi ya jeshi ya Ménaka kaskazini mashariki mwa Mali kwenye picha iliyopiwa Juni 13, 2022.
Wanajeshi wakipata mafunzo katika kambi ya jeshi ya Ménaka kaskazini mashariki mwa Mali kwenye picha iliyopiwa Juni 13, 2022. © AFP PHOTO / Etat Major des Armees
Matangazo ya kibiashara

Hali ya usalama imezorota kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miezi minane iliyopita katika maeneo ya Ménaka na Gao kufuatia mashambulizi ya kundi lenye mfungamano na Islamic State katika Sahara Kubwa (EIGS), zaidi ya iliyokuwa eneo lake la hatua na ushawishi.

Wanajihadi wamepigana kwa siku kadhaa katika miji kadhaa ya mkoa wa Ménaka", amebainisha afisa aliyechaguliwa wa eneo hilo kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu za usalama, habari zilizothibitishwa kwa shiika la habari la AFP na afisa mwingine aliyechaguliwa wa eneo hilo aliyoko mjini Bamako na chanzo cha usalama kutoka Magharibi huko Niamey.

Hakuna anayetaja idadi ya vifo, wala kutoa kiwango cha mapigano haya. Hii ni ngumu sana kwa kukosekana kwa taarifa za kuaminika kutoka kwa maeneo ambayo hayafikiki kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande mwingine, makundi ya wanajihadi yanayoshirikiana na Al-Qaeda na EIGS yalitoa tathmini nzito sana katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa chombo chao cha propaganda kilichonukuliwa na kituo cha Marekani cha kufuatilia maeneo ya wanajihadi, SITE.

Siku ya Jumatatu kundi la EIGS lilisema kwamba liliwaua wapiganaji 40 kutoka kundi linalodai Kusaidia Uislamu na Waislamu (GSIM, JNIM kwa Kiarabu) katika mkoa wa Ménaka, na baadaye kundi hili la GSIM limejibu Jumanne kuwa liliua Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi zaidi ya wapiganaji 70 wa kundi la EIGS, kisha likakiri kuwa limepoteza takriban wapiganaji thelathini.

Eneo hili kubwa la mbali limekuwa eneo la mapigano kwa miezi kadhaa kati ya makundi haya hasimu ya kijihadi, na mapigano kati ya wanajihadi na hasa makundi yenye silaha ya Tuareg ambao walitia saini mikataba ya amani na serikali mwaka 2015. Eneo hilo pia linakabiliwa na ujambazi na biashara haramu. Raia wengi wamepata kimbilio katika mji wa Ménaka.

Raia wawili, akiwemo mtoto, pia waliuawa katika shambulio la watu wenye silaha kwenye basi la usafiri wa umma kati ya mitaa ya Ansongo na Ménaka, polisi imesema Jumanne.

Mapigano kati ya EIGS na kitengo cha Kundi la Kujilinda la Tuareg Imghads na Washirika wake (GATIA) pia yaliripotiwa Jumatatu katika mkoa wa Gao katika wilaya ya Anchwadj, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka muugano wa makundi wa Juni 14, 2014 kutoka Algiers , ambao GATIA ni mwanachama wake. 

Kundi hili la GATIA linadai kuwa mashambulizi haya yalisababisha takriban vifo kumi na tano kwa upande wa EIGS, tisa upande wa muungano, pamoja na raia wanne waliouawa na EIGS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.