Pata taarifa kuu

Mlinda amani wa nne wa Chad auawa na kilipuzi kaskazini mwa Mali

Mlinda amani wa nne wa Chad amefariki kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa kilipuzi kaskazini mwa Mali, amesema Jumanne msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSMA).

Askari wa MINUSMA akishika doria karibu na Msikiti Mkuu wa Timbuktu, Desemba 9, 2021.
Askari wa MINUSMA akishika doria karibu na Msikiti Mkuu wa Timbuktu, Desemba 9, 2021. © AFP - FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao waliuawa baada ya gari lao kukanya kilipuzi (IED) siku ya Jumatatu walipokuwa kwenye doria ya kutegua mabomu huko Tessalit, katika mkoa wa Kidal. Wengine wawili walijeruhiwa vibaya.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres "analaani vikali" shambulio hilo, msemaji wake Stéphane Dujarric amesema katika taarifa iliyotolewa mjini New York. Bwana Guterres anatoa "rambirambi zake za dhati" kwa Chad na anatoa masikitiko yake kwa familia za wahanga.

Mashambulizi dhidi ya walinda amani yanaweza kujumuisha uhalifu wa kivita chini ya sheria za kimataifa, amesema Bw. Guterres.

Vilipuzi vilivyoboreshwa vimesababisha vifo vya walinda amani 76 tangu kuanza kwa misheni hiyo mnamo 2013, MINUSMA imesema.

Mali imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya wanajihadi na ghasia za kila aina tangu mwaka wa 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.