Pata taarifa kuu

Marekani: Usalama nchini Mali umedorora licha ya kuwasili kwa Wagner

Marekani inachukulia kwamba usalama umezorota sana nchini Mali tangu jeshi la serikali lilipitisha mamluki wa kampuni ya Wagner ya Urusi, ambao uwepo wao unazuia sana hatua ya Marekani dhidi ya wanajihadi, afisa mmoja mkuu amesema siku ya Jumatano.

Hifadhi kwenye kumbukumbu Aprili 2022. Kaskazini mwa mali, inayokaliwa na mamluki kutoka Urusi.
Hifadhi kwenye kumbukumbu Aprili 2022. Kaskazini mwa mali, inayokaliwa na mamluki kutoka Urusi. AP
Matangazo ya kibiashara

"Wanajeshi wa Mali waliwaleta mamluki wa Wagner na ugaidi ukazidi kuwa mbaya," Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Victoria Nuland alisema katika mkutano wa video, akirejea kutoka ziara yake katika uka,da wa Sahel, ikiwa ni pamoja na Mali kati ya Oktoba 16 na 20. Aliripoti ongezeko la takriban 30% la vitendo vya kigaidi katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Maneno haya yanakinzana na yale ya wanajeshi waliochukua madaraka kwa nguvu mwaka 2020 nchini humo waliotikiswa tangu 2012 na ghasia na kuenea kwa wanajihadi. Mamlaka ya Mali imegeuka kwa mwaka mmoja kutoka kwa mshirika wa Ufaransa na washirika kugeukia Urusi. Wanarudia kusema kwamba wamegeuza mwelekeo wa usalama na wamevishinda vikundi vya jihadi.

Marekani, Ufaransa na nchi za Wamagharibi wanashutumu utawala wa kijeshi kwa kusajili huduma za kampuni ya usalama ya Wagner, katika hatua hizo zilizokataliwa. Wakuu wa Mali wanakanusha hili na wanazungumza juu ya ushirikiano na jeshi la Urusi kwa jina la uhusiano wa zamani wa serikali na serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.