Pata taarifa kuu

Bamako yaweka masharti kurejesha uhusiano na Ufaransa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop amesema leo Jumanne kwamba utawala wa huko Bamako unaoongozwa na idadi kubwa ya wanajeshi umeweka masharti ya kurejesha uhusiano na Ufaransa kwa kuwepo na heshima kwa "utawala" wake na "chaguo zake za kimkakati".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop, hapa alikuwa Moscow Novemba 11, 2021.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop, hapa alikuwa Moscow Novemba 11, 2021. Β© Yuri Kochetkov / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mali inataka mamlaka yetu kuheshimiwa, na kwamba uchaguzi wetu wa kimkakati na chaguo letu la washirika kuheshimiwa, na kwamba maslahi muhimu ya raia wa Mali yazingatiwe," amesema Bw. Diop katika Kongamano la 8 la Kimataifa la Dakar, mkutano kuhusu usalama na amani barani Afrika, kuelezea kuzorota kwa kikatili kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbil, hali ambayo ilisababisha wanajeshi wa Ufaransa kuondoka Mali mnamo mwezi wa Agosti baada ya miaka tisa ya mapigano dhidi ya wanajihadi.

"Ikiwa vipengele hivi vitazingatiwa, Mali haina tatizo kushirikiana na mshirika yeyote, ikiwa ni pamoja na Ufaransa," amewahakikishia waandishi wa habari.

Alipoulizwa kuhusu shutuma zake dhidi ya Ufaransa katika barua iliyotumwa mwezi Agosti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikilaani hasa "ukiukaji wa mara kwa mara wa anga ya Mali unaofanywa na vikosi vya Ufaransa, Bw. Diop amethibitisha kuwa nchi yake inasubiri kikao maalum ili aweze kutoa uthibitisho.

Mali si mtoto, sisi ni wanachama wa Umoja wa Mataifa, tunajua sheria. Tumeomba kikao maalum ili kuweza kujadili suala hili,” amesema.

"Wale walio kinyume wanaogopa nini? Ikiwa hatuna uthibitisho, tuitishe kikao", ameongeza mkuu wa diplomasia ya Mali.

Katika barua yake, alidai kuwa mamlaka ya Mali ina "vielelezo kadhaa vya ushahidi kwamba ukiukaji huu wa wazi wa anga ya Mali umetumiwa na Ufaransa kukusanya taarifa za kijasusi kwa manufaa ya makundi ya kigaidi yanayoendesha shughuli zao katika ukanda wa Sahel na kuwaachia silaha na risasi". madai yaliyokanushwa na Ufaransa.

"Kilicho muhimu ni kwamba washirika wetu wanakuja kwa nia ya kufanya kazi nasi kwa suluhu, na sio kuja kutuamuru suluhu," Bw. Diop pia amebaini.

"Hatupaswi kulaani watu, tuna wajibu wetu wenyewe", hata hivyo amekiri katika hotuba yake mbele ya Jukwaa la Dakar.

"Tumeshindwa katika ushirikiano wa bara, tumeshindwa kuimarisha ushirikiano kati yetu, tumeshindwa katika jukumu letu la kuhakikisha usalama wetu na ninaamini kwamba hatuwezi kuwajibika kwa hilo na wengine," amehitimisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.