Pata taarifa kuu

Umoja wa Afrika walaani mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), Moussa Faki Mahamat, amelaani "mabadiliko ya serikali yaliyo kinyume cha katiba" nchini Burkina Faso baada ya jeshi kumuondoa mamlakani Luteni Kanali Paul-Henri.Moussa Faki Mahamat ametaka "kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba kabla ya Julai 1, 2024".

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat.
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat. © Dursun Aydemir/Anadolu Agency via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

"Mwenyekiti anatoa wito kwa wanajeshi kujiepusha mara moja na kitendo chochote cha vurugu au vitisho kwa raia, uhuru wa umma, haki za binadamu," AU mesema katika taarifa yake fupi.

Mwenyekiti wa Tume ya AU hatimaye ametoa wito wa "kufuatwa kikamilifu kwa makataa ya uchaguzi kwa kurejea kwa utaratibu wa kikatiba kabla ya Julai 1, 2024".

Baada ya siku moja yenye vurugu na milio ya risasi katika mji mkuu wa Ouagadougou, kundi la wanajeshi walijitokeza kwenye televisheni ya Burkina Faso kutangaza kutimuliwa mamlakani kwa Kanali Damiba, na nafasi yake kuchukuliwa na Kepteni Ibrahim Traoré, 34.

Utawala mpya wa kijshi umesitisha katiba na kuvunja serikali na bunge, bila kutangaza kuhusu ratiba ya mpito ambayo ilikuwa suala la makubaliano na ECOWAS na kutangazwa kurejeshwa kwa mamlaka ya kiraia mnamo mwezi wa Julai 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.