Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Burkina Faso: 'Mgogoro wa ndani katika jeshi', mazungumzo yanayoendelea

Hali nchini Burkina Faso ambako milio ya risasi ilisikika na wanajeshi kupiga kambi siku ya Ijumaa kwenye barabara kuu za mji mkuu Ouagadougou, inahusishwa na "mgogoro wa ndani katika jeshi", msemaji wa serikali ya Burkina Faso ameliambia shirika la habari la AFP.

"Majadiliano yanaendelea". "Rais", Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, "yuko na watu wake na wanaongoza majadiliano", kwa mujibu wa Bw. Bilgo.
"Majadiliano yanaendelea". "Rais", Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, "yuko na watu wake na wanaongoza majadiliano", kwa mujibu wa Bw. Bilgo. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya kijeshi iliyo madarakani inajikuta ikikabiliwa na malumbano ya ndani katika jeshi lake. Jeshi lilichukua madaraka mwez wa Januari mwaka huu kwa kupitia mapinduzi ya kijeshi ambayo yalianza baada ya kambi kadhaa za kijeshi kuasi.

Kabla ya mapambazuko siku ya Ijumaa katika mji mkuu wa Ouagadougou, milio ya risasi ambayo bado haijafahamika asili yake ilisikika katika eneo kunakopatikana ikulu ya rais na makao makuu ya jeshi madarakani tangu mwezi wa Januari, mashuhuda wameliambia shirika la habari la AFP.

"Ni mzozo wa ndani katika jeshi, majadiliano yanaendelea ili kupata muafaka," amesema Bw. Bilgo, baada ya serikali kukaa kimya kwa saa kadhaa.

Ni "mgogoro wa kijeshi wa wa baadhi ya kambi, kulingana na madai yanayohusiana na marupurupu na baadhi ya mishahara", ameongeza Bw. Bilgo.

"Majadiliano yanaendelea," amebaini. "Rais", Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, "yuko na watu wake na wanaongoza majadiliano", kwa mujibu wa Bw. Bilgo.

Mapinduzi yaliyoongozwa mwezi Januari na Luteni Kanali Damiba yalimpindua Rais mteule Roch Marc Christian Kaboré.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.