Pata taarifa kuu

Ouagadougou yaingia tena katika machafuko

Inaonekana wanajeshi ambao wamesalia watiifu kwa Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba wanataka kuvamia mji mkuu. Vikosi vya usalama vilivyojihami vikali vimetumwa Jumamosi saa sita mchana katikati mwa mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, na katika maeneo kadhaa ya kimkakati katika mji mkuu wa Burkina Faso na baadhi ya barabara zimefungwa. 

Mbele ya makao makuu ya televisheni ya taifa ya Burkina Faso, mjini Ouagadougou, tarehe 1 Oktoba 2022.
Mbele ya makao makuu ya televisheni ya taifa ya Burkina Faso, mjini Ouagadougou, tarehe 1 Oktoba 2022. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Mashahidi wanabaini kwamba wameona wanajeshi wakitumwa kuelekea televisheni ya taifa, ambapo vizuizi vimewekwa kwenye barabarani. Hivi ndivyo hali ilivyo pia katika eneo la Ouaga2000, ambapo kunapatikana ikulu ya rais ya Kosyam.

Wafanyabiashara katika soko kuu wamefunga shughuli zao na baadhi ya maeneo maarufu yanayotembelewa na watu wengi yamekuwa tupu.

Siku moja kabla, wanajeshi walitangaza kwenye televisheni ya taifa kwamba Kapteni Ibrahim Traoré, 34, ndie kiongozi mpya, ambaye anachukuwa nafasi ya Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba. Lakini inaonekana wanajeshi ambao wamesalia watiifu kwa Rais Paul-Henri Sandaogo Damiba wanataka kuvamia mji mkuu.

Kwenye video zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii, wakaazi wa mji wa Ouagadougou wamefunga shughuli zao mapema na kuharakia kwenda nyumbani kwao, wakihofia mapigano kati ya wanajeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.