Pata taarifa kuu
MAPINDUZI-USALAMA

Burkina: Wanajeshi watangaza kuvunjwa kwa serikali, Kapteni Ibrahim Traoré achukua mamlaka

Kundi la wanajeshi lilitangaza Ijumaa kwenye televisheni ya taifa nchini Burkina Faso kutengwa kwa kiongozi wa serikali ya kijeshi Paul-Henri Damiba, aliye kuwa madarakani tangu mapinduzi ya mwezi wa Januari.

Kundi la wanajeshi linatangaza kwenye televisheni ya taifa ya Burkina Faso kutengwa kwa kiongozi wa utawala wa kijeshi, Paul-Henri Damiba, Ijumaa hii, Septemba 30, 2022 huko Ouagadougou.
Kundi la wanajeshi linatangaza kwenye televisheni ya taifa ya Burkina Faso kutengwa kwa kiongozi wa utawala wa kijeshi, Paul-Henri Damiba, Ijumaa hii, Septemba 30, 2022 huko Ouagadougou. © RTB / Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao waliofanya mapinduzi pia walitangaza kuvunjwa kwa serikali na Katiba, pamoja na kufungwa kwa mipaka ya nchi hadi hapo itakapotangazwa tena. Kiongozi mpya mwenye nguvu nchini Burkina Faso, rais mteule wa MPSR, sasa ni Kepteni Ibrahim Traoré.

Luteni Kanali Damiba haongozi tena kipindi cha mpito nchini Burkina Faso. Nafasi yake inachukuliwa na Kapteni Ibrahim Traoré ambaye anaongoza Vuguvugu la Patriotic for Safeguard and Restoration (MPSR), ambalo lilianzishwa wakati wa mapinduzi ya awali mwezi Januari mwaka huu na ambalo jina lake halibadiliki.

Mipaka ya nchi kavu na anga imefungwa kuanzia saa sita usiku saa za nchini Burkina Faso, Katiba imesitishwa na serikali imevunjwa. Sheria ya kutotoka nje pia imetangazwa, kati ya saa tatu usiku na saa kumi namoja alfajiri.

Shughuli zote za kisiasa na za kiraia zimesitishwa na "wadau katika siasa " hivi karibuni vitaitwa kuandaa hati mpya ya mpito ili kumteua rais mpya, "raia au mwanajeshi", viongozi wapya wa kijeshi wamebainisha. 

Wanajshi hao pia wamehakikishia jumuiya ya kimataifa kwamba ahadi za Burkina Faso zitaheshimishwa, "hasa ​​haki za binadamu", kulingana na taarifa iliyosomwa kwenye televisheni.

Hatima ya Luteni Kanali Damiba haijabainishwa. Akijibu uvumi unaoenea kwenye mitandao ya kijamii, chanzo cha kidiplomasia cha Ufaransa kimefafanua kuwa jeshi la Ufaransa halimlindi wala kulijampa hifadhi yoyote Luteni Kanali Damiba.

Lakini kwa sasa, maswali yanaendelea sio tu juu ya hatima ya Luteni Kanali Damiba lakini pia juu ya majibu ya wale ambao, hasa ndani ya jeshi, wanaweza kuamua kubaki waaminifu kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.