Pata taarifa kuu
RWANDA-USHIRIKIANO

Rais wa Rwanda azitaka nchi nyingine kusaidia Msumbiji kukabiliana na mdororo wa usalama

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametembelea vikosi vya nchi yake, Kaskazini mwa Msumbiji, vinakopambana na wapiganaji wa kijihadi wenye mafungamano na kundi la Islamic State, IS.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na rais wa Rwanda Paul Kagame wakitembea pamoja wakati wa ukaguzi wa vikosi vya usalama vya Msumbiji na Rwanda huko Pemba, Msumbiji, Septemba 24, 2021
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na rais wa Rwanda Paul Kagame wakitembea pamoja wakati wa ukaguzi wa vikosi vya usalama vya Msumbiji na Rwanda huko Pemba, Msumbiji, Septemba 24, 2021 REUTERS - BAZ RATNER
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Julai, Rwanda ilikuwa nchi ya kwanza kutuma wanajeshi wake zaidi ya 1,000 katika mkoa wa Cabo Delgado na imefanikiwa kudhibiti eneo na kuwarudisha nyuma wapiganaji hao.

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema wanajeshi wake hawawezi kubakia milele katika jimbo la Msumbiji la Cabo Delgado, wakati ukifika wataondoka, amebaini.

« Ni jukumu la Msumbiji kuamua ni kwa muda gani wanawahitaji wanajeshi wa Rwanda kubakia nchini humo. Natoa wito kwa nchi nyingine kuisadia Msumbiji », amesema rais Paul kagame katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi huko Pemba, mji mkuu wa jimbo la Cabo Delgado.

Wanajeshi hao wa Rwanda wamekuwa wakishirikiana na wanajeshi wa Msumbiji tangu mwezi Julai, kurejesha udhibiti wa maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na wanamgambo wenye itikadi kali za kidini wenye mafungamano na kundi la Islamic State.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame akizungumza na wanajeshi wa nchi yake baada ya kuwatembelea katika mkoa wa Cabo Delgado nchini Msumbiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.