Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-USALAMA

SADC yazindua ujumbe wa kijeshi kuisaidi Msumbiji

Jumuiya ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, imezindua kikosi cha pamoja cha wanajeshi, kuisadia Msumbuji kupambana na wanajihadi  Kaskazini mwa nchi hiyo, eneo lenye utajiri wa gesi.

Wanajeshi wa Rwanda waingia Msumbiji, kwa ombi la Rais Nyusi, Julai 10, 2021.
Wanajeshi wa Rwanda waingia Msumbiji, kwa ombi la Rais Nyusi, Julai 10, 2021. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho kimezinduliwa katika mji wa Pemba, makao makuu ya mkoa wa Cabo Delgado, wakati huu kikosi cha wanajeshi wa Rwanda wapatao 1000 kikisema kinapiga hatua kubwa dhidi ya majihadi.

Mwishoni mwa mwezi wa Julai, nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zilitangaza kutuma wanajeshi kusaidia jeshi la Msumbiji katika vita vyake dhidi ya wanajihadi wanaoendesha ukatili wao kaskazini mwa nchi, eneo lenye utajiri wa gesi.

Uzinduzi wa kikosi hiki cha SADC unakuja siku moja baada ya wanajeshi wa Msumbiji na Rwanda kudhibiti eneo hilo kutoka mikononi mwa wanajihadi hao.

Vikosi vya Msumbiji vikisaidiwa na wanajeshi wa Rwanda vimewafurusha wanamgambo wa itikadi kali waliokuwa wanaudhibiti mji muhimu wa bandari wa Mocimboa da Praia eneo la kaskazini mwa nchi hiyo lenye utajiri wa gesi

Msemaji wa Wizara ya ulinzi ya Msumbiji Kanali Omar Saranga alisema katika kikao cha waandishi wa habari mjini Maputo kuwa sasa wanayadhibiti majengo ya serikali, bandari, uwanja wa ndege, hospitali na vituo vingine muhimu. Mji wa Mocimboa da Praia ambako mashambulizi ya kwanza ya itikadi kali yalifanywa Oktoba 2017, tangu mwaka jana umetumika kama makao makuu ya wapiganaji wenye mahusiano na Kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS, wakijiita Al-Shabaab nchini humo.

Msemaji wa jeshi la pamoja Kanali Ronald Rwivanga amesema mji huo wa bandari ulikuwa ngome ya mwisho ya wanamgambo hao na kukombolewa kwake kunaashiria mwisho wa awamu ya kwanza ya operesheni za kupambana na uasi wa itikadi kali.

Wanajeshi wa Msumbuji wamekuwa wakipambana kukamata udhibiti wa mkoa wa Cabo Delgado, eneo lenye mojawapo ya miradi mikubwa zaidi ya gesi asilia – mradi wa dola bilioni 20 unaoendeshwa na kampuni kubwa ya nishati ya Total ya Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.