Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-USALAMA

Msumbiji: Vikosi vya Rwanda vyalidhibiti tena eneo la Mocimboa da Praia

Nchini Msumbiji, jeshi la Rwanda limetangaza kwenye Twitter Jumapili alasiri, Agosti 8, kwamba kwa ushirikiano na vikosi vya Msumbiji, vimeudhbiti tena mji wa kimkakati wa Mocimboa da Praia kutoka mikononi mwa wanajihadi.

Wanajeshi wa Rwanda kutoka Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) nchini Msumbiji, wakati kiondoka uwanja wa ndege wa Kanombe, Kigali, Rwanda, Julai 10, 2021.
Wanajeshi wa Rwanda kutoka Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) nchini Msumbiji, wakati kiondoka uwanja wa ndege wa Kanombe, Kigali, Rwanda, Julai 10, 2021. AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Kwa wiki kadhaa, wanajeshi elfu wa Rwanda wametumwa katika mkoa wa Cabo Delgado kusaidia Maputo kusitisha kusonga mbele kwa waasi hawa wanaofungamana na kundi la Islamic State.

Mocimboa da Praia ni mji wa kimkakati, kwa sababu ni mji wa bandari, ulio kwenye Bahari ya Hindi, na ambao kwa hivyo ulikuwa chanzo muhimu cha kupata msaada wa chakula na risasi kwa waasi. Mji huo ulikuwa hata moja ya ngome zao kuu kwa miezi mingi. Lengo la jeshi la Rwanda kwa ushirikiano na vikosi vya jeshi vya Msumbiji ilikuwa kuudhibiti.

Wanyarwanda, ambao wanaonesha kupelekwa kwao kama mafanikio, pia walitangaza siku chache zilizopita kuwa walishiriki kudhibiti tena mji mwingine, wa Afungi, ambao ni makao mkuu ya kampuni ya Ufaransa TOTAL, inaendesha mradi mkubwa wa bilioni 17.

Sio tu vikosi vya Rwanda viko nchini Msumbiji. Botswana tayari imetuma wanajeshi wake ncvhini humo na Afrika Kusini imetangaza kutuma wanajeshi 1,500 kusaidia kusitisha mashambulio ya wanajihadi huko Cabo Delgado ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali na kusababisha zaidi ya watu 800,000 kuyatoroka makaazi yao, kulingana na mamlaka nchini Msumbiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.