Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-USALAMA

SADC kupeleka wanajeshi wa jumuiya hiyo maeneo ya mipaka kati ya Msumbiji na Tanzania

Mataifa ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC, yamekubaliana kutuma wanajeshi nchini Msumbiji kukabiliana na wanajihadi katika mkoa wa Cabo Delgado ambao unashuhudia changamoto za kiusalama, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mkutano wa viongozi wa SADC kuhusu hali ya uchaguzi wa DRC mjini Brazzaville desemba 26 2018
Mkutano wa viongozi wa SADC kuhusu hali ya uchaguzi wa DRC mjini Brazzaville desemba 26 2018 Reuters/Bouka Roch
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, haijafahamika kwa kina kuhusu kikosi hicho na muda ambao kitatumia kukabiliana na manajihadi hao, lakini mapema mwaka huu, iliropotiwa kuwa SADC inatarajiwa kutuma wanajeshi 3,000 nchini humo.

Mwenyeji wa mkutano huo, rais Filipe Nyusi wa Msumbiji ambaye pia ni mwenye kiti wa sasa wa Jumuiya ya SADC aliitisha mkutano huo ili kuomba usaidizi wa  marais wenzake kuhusu kitisho cha wanamgambo wanaohusishwa na kundi linalojiita Islamic State IS, ambao wamekuwa wakiendesha mashambulizi katika jimbo la Capo Delgado,kaskazini mwa Msumbiji

Katibu mtendaji wa jumuiya ya SADC, Stragomena Pax amesema marais hao wamekubaliana kupeleka kikosi cha pamoja cha jumuiya hiyo nchini Msumbiji ili kuimarisha usalama wa eneo hilo, huku wakitoa wito wa kupewa msaada wa kimataifa katika mapambano yake dhidi ya ugaidi.

Wapiaganaji wa kigaidi wameshutumiwa kwa kufanya mauaji ya kikatili tangu mwaka 2017 kwa kufanya uvamizi wa vijiji na miji maeneo ya mpaka kati ya Msumbiji na Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.