Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-USALAMA

SADC kuimarisha Usalama katika eneo la mpakani kati ya Tanzania na Msumbiji

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC, wamekutana kwa dharura mjini Maputo, Msumbiji, ambapo wamejadili hali ya usalama kwenye mataifa yao na kitisho cha makundi ya kijihadi kaskazini mwa nchi ya Msumbiji.

Nembo ya Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC
Nembo ya Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC (Source : www.sadc.int)
Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho ni mfululizo wa vikao cya wakuu wa nchi za SADC ambao mwezi mmoja uliopita walikutana tena mjini Maputo lakini wakashindwa kutoka na maazimio kuhusu namna ya kukabiliana na makundi ya kijihadi yanayoendelea kukua katika baadhi ya nchi wanachama.

Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo rais wa Msumbiji, Phillipe Nyusi ambaye ndiye mwenyekiti wa SADC amesema Jumuia hiyo ya Kiuchumi ya Kusini mwa Afrika, itakuwa mstari wa mbele katika katika mapambano dhidi ya ugaidi, ambao umekithiri katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, pamoja na kuweka wazi mikakati ya Jumuia hiyo kusaidia kupambana na magaidi ambao wamejikita katika jimbo la Cabo Delgado nchini mwake.

Wajumbe waliohudhuria mkutano huu hata hivyo wamepongeza  juhudi kubwa ambazo zimepigwa katika kutokomeza ugaidi kwenye eneo hilo licha ya kuwa bado hali ya baadaye ni ya wasiwasi, ambapo wamejadili kuhusu uchumi wan chi zao ambazo zimeathiriwa kufuatia janga la Corona.

Mkutano huo wa dharura ni wa kwanza kuhudhuriwa na Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan tangu azishike hatamu za uongozi wan chi yake mwezi Machi mwaka huu kufuatia kifo cha mtangulizi wake, John Magufuli

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.