Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Visa vya utekaji nyara vyaibua hasira miongoni mwa raia Nigeria

Operesheni ya uokoaji inaendelea kujaribu kuwapata wasichana wadogo 317 ambao walikamatwa katika shule yao ya bweni katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Mmoja wa wazazi aliyempata mwanae ambaye alikuwa ametekwa nyara kwa wiki moja na Boko Haram mnamo Desemba 18, 2020 huko Katsina.
Mmoja wa wazazi aliyempata mwanae ambaye alikuwa ametekwa nyara kwa wiki moja na Boko Haram mnamo Desemba 18, 2020 huko Katsina. © AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa jimbo la Zamfara wamepandwa na hasira kutokana na kuongezeka kwa visa hivyo vya utekaji nyara. Magari kadhaa yaliharibiwa, na mwandishi wa habari mmoja alijeruhiwa huko Jangebe baada ya watu kadhaa kurusha mawe Ijumaa wiki hii katika makabiliano na polisi wakisema sewrikali ya jimbo hilo haifanyi chochote kukomesha visa hivyo ambavyo vimekuwa vijirudi mara kwa mara.

Raia wamekasirishwa na hali hiyo kutokana na kushindwa kwa mamlaka kulinda usalama wa wananche wake.

Hii ni mara ya tatu tangu mwezi Desemba shule inashambuliwa usiku na watu wenye silaha, na wanafunzi wanatekwa nyara.

Kuanzia mwezi Desemba wanafunzi 344 wa shule ya upili walitekwa nyara huko Katsina kabla ya kuachiliwa wiki moja baadaye. Wiki iliyopita, watu 42 wakiwemo wanafunzi 27 walitekwa nyara katika jimbo la Niger.

Wazazi wa wanafunzi karibu 50 ambao walifanikiwa kutoroka walikataa kuwaruhusu watoto wao kuendelea kuhojiwa na idara za usalama.

Buhari onya makundi ya uhalifu

Ijumaa jioni, rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema utawala wake "hautakubali majambazi kuendelea kuwahujumu wananchi wake".

Katika taarifa, rais Buhari alihakikisha kuwa vikosi vya usalama vina uwezo wa kutumia "nguvu kubwa" dhidi ya makundi ya wahalifu, lakini kutokana na mateka wanaoshikiliwa "ambao wanaweza kutumika kama ngao kwa makundi hayo" hali hiyo inasababisha wajizuie kutumia nguvu.

Rais wa Nigeria pia alionya magavana wa eneo hilo ambao wamezoea kufanya mazungumzo na viongozi wa makundi ya wahalifu na kuamini wananunua amani kwa kuwapa "pesa na magari". "Inaweza kuwa na athari mbaya katika siku za usoni," alionya rais wa Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.