Pata taarifa kuu
NIGERIA

Buhari awafuta kazi baadhi ya wakuu wa jeshi

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amewafuta kazi wakuu wa vikosi vya wanajeshi wa nchi hiyo ambao aliwateua wakati alipoanza kazi mnamo mwaka wa 2015.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari Nigeria Presidency/Handout / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hakuna sababu iliyotolewa ya kupigwa kalamu kwa maafisa hao.

Hatua hii inakuja wakati taifa hili la Nigeria linaendelea kukabiliana na ukosefu wa usalama ulioenea ikiwa ni pamoja na uasi wa muda mrefu wa Boko Haram na utekaji nyara uliokithiri.

Hali ya usalama nchini Nigeria imeendelea kudorora kutokana na makundi ya wanamgambo wa Kiislamu, hasa kundi hili la Boko Haram ambalo linaendesha mashambulizi yake nchini Nigeria na katika nchi jirani.

Vikosi vya usalama na jeshi vimekuwa vikilengwa katika mashambulizi hayo ambayo yameuawa waelfu ya watu kufikia sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.