Pata taarifa kuu
LIBYA-QATAR-UTURUKI-USALAMA-SIASA

Tripoli, Uturuki na Qatar waafikiana kuhusu ushirikiano wa kijeshi

Serikali ya umoja wa kitaifa inaotambuliwa na Umoja wa Mataifa nchini Libya (GNA), imesaini mkataba wa kijeshi na serikali za Uturuki na Qatar kuhusu ushirikiano wa kijeshi.

Wapiganaji wanaounga mkono serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli, Juni 4, 2020.
Wapiganaji wanaounga mkono serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli, Juni 4, 2020. REUTERS/Ayman Al-Sahili
Matangazo ya kibiashara

Chini ya mkataba huo Uturuki na Qatar zitajenga taasisi ya mafunzo ya kijeshi na kuwatuma washauri wa kijeshi nchini Libya.

Kulingana na mkataba huo kituo hicho cha kijeshi cha Uturuki na Qatar kitajengwa katika Bandari ya Misrata nchini Libya.

Nchi hizo tatu pia zimeafiki kuwa kutakuwa kukifanyika mkutano kila mwezi katika ngazi ya wakuu wa majeshi ya Libya, Qatar, na Uturuki katika Bandari ya Misrata.

Mwezi Novemba 2019, seikali ya Uturuki na serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli (GNA) zilisaini mkataba wa ushirikiano wa kijeshi na pia katika masuala ya mipaka ya baharini, mashariki mwa Mediterania.

Hivi karibuni Uturuki ilishtumiwa kuingilia uchumi wa Libya kwenye bandari ya Tripoli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.