Pata taarifa kuu
LIBYA-UTURUKI-UCHUMI

Libya: Uturuki yashtumiwa kuingilia uchumi wa Libya kwenye bandari ya Tripoli

Zoezi la kusaini mikataba ya kiuchumi na kibiashara kati ya Ankara na Tripoli linashika kasi. Waziri wa Biashara wa Uturuki Ruhsar Pekcan amebaini kwamba nchi yake imesaini 'mikataba muhimu sana ya kiuchumi na biashara na serikali ya Sarraj'.

Kampuni moja ya Uturuki imepewa majukumu ya kusimamia shughuli zote za bandari ya Tripoli, Libya.
Kampuni moja ya Uturuki imepewa majukumu ya kusimamia shughuli zote za bandari ya Tripoli, Libya. Mahmud TURKIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri Ruhsar Pekcan ameyasema hayo jana Alhamisi akiambatana na Waziri wa Mipango wa Libya Tahar Jouhaimi wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Walisaini mkataba juu ya kuanza tena kwa miradi kadhaa ya kampuni za Uturuki zilizosimamishwa kwa sababu ya hali ya usalama nchini Libya.

Mkataba mwengine uliyosainiwa mapema, ambao unaruhusu kampuni ya Uturuki kusimamia bidhaa kutoka nchi za kigeni kwenye bandari ya Tripoli, sasa umeibua wasiwasi mkubwa nchini Libya.

Kampuni hiyo ya SCK, yenye makao yake makuu huko Istanbul inamilikiwa na mfanyabiashara Mehmet Kocabasa, rafiki wa rais Erdogan. Kampuni hii ya Uturuki sasa imepewa jukumu na Serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) huko Tripoli kusimamia uagizaji wa baharini hadi bandari ya mji mkuu Tripoli kwa niaba ya mamlaka ya forodha ya Libya.

Kampuni hiyo ilisaini mkataba wa miaka minane kufanya kazi hiyo na serikali ya umoja wa kitaifa kupitia Waziri wake wa Fedha Faraj Boumtari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.