Pata taarifa kuu
AU-WAHAMIAJI-USALAMA

Umoja wa Afrika wakubaliana kushughulikia suala la wahamiaji

Viongozi wa Umoja wa Afrika wamekubaliana kuunda bodi maalum itakayosaidia, kushughulikia masuala ya wahamiaji lakini pia kuthathmini sera za uhamiaji katika mataifa ya Afrika.

Viongozi wa Umoja wa Afrika wakutana Mauritania katika kikao 31 cha Umoja wa Afrika.
Viongozi wa Umoja wa Afrika wakutana Mauritania katika kikao 31 cha Umoja wa Afrika. Ahmed OULD MOHAMED OULD ELHADJ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tume hiyo pia inatarajiwa kutafuta mbinu za kuimairisha uhusiano kati ya mataifa ya kigeni kuhusu masuala ya uhamiaji.

Hii imekuja wakati huu waafrika wengi wakiendelea kukimbilia barani Ulaya, huku wengi wakizama katika Bahari ya Mediterania wakiwa njiani.

Hayo yanajiri wakati ambapo wahamiaji 63 wamezama katika Bahari ya Meditterenian Pwani ya Libya, wakiwa njiani kwenda barani Ulaya.

Hata hivyo, wahamiaji wengine 41 waliokolewa, katika meli hiyo iliyokuwa na abiria zaidi ya 100.

Kati ya siku ya Ijumaa na Jumamosi wiki, iliyopita, mamia ya wahamiaji walizama na maafisa wanasema zaidi ya 100 hawajapatikana.

Raia wengi kutoka Afrika ambao wamekua wakielekea ulaya kutafuta maisha mazuri walikumbwa na mikasa mingi, huku baadhi yao wakipoteza maisha kutokana na jali mbalimbali zilizokua zikiwakumba katika maeneo wanakopita hasa baharini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.