Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA

Mamia ya waandamanaji wa upinzani wakamatwa Zambia

Polisi nchini Zambia wamewakamata waandamanaji zaidi ya 130 wa upinzani waliokuwa wanaandamana  kupinga ushindi wa rais Edgar Lungu baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu uliofanyika  wiki iliyopita.

Polisi wa kutuliza ghasia wakipiga kambi mjini Livingstone
Polisi wa kutuliza ghasia wakipiga kambi mjini Livingstone enca.com
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi siku ya Jumanne, ilimtangaza Lungu mshindi baada ya kupata asilimia 50.35 ya kura zote zilizopigwa huku mpinzani wake wa karibu Hakainde Hichilema akiwa wa pili kwa asilimia 47.63.

Ripoti zinasema kuwa, maandamano hayo yalitokea katika mji wa utalii wa Livingstone Kusini mwa nchi hiyo kwa mujibu wa Kamada wa polisi Godwin Phiri ambaye ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters.

Chama cha upinzani cha UPND kimekataa kutambua matokeo hayo na kudai kuwa kura ziliibiwa na inapanga kwenda katika Mahakama ya Kikatiba kupinga ushindi wa rais Lungu.

Hata hivyo, madai ya chama hiki cha upinzani yamekanushwa vikali na Tume ya Uchaguzi na chama tawala cha PF.

Wafuasi wa rais Lungu, wameendelea kusherehekea ushindi wa kiongozi wao ambaye anatarajiwa kuapishwa baada ya wiki moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.