Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA

Maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Nkurunziza yaendelea

Maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza yameendelea mjini Bujumbura, nchini Burundi.

Waandamanaji wanasema kwamba kulingana na Katiba ya Burundi, Rais Pierre Nkurunziza hawezi kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanasema kwamba kulingana na Katiba ya Burundi, Rais Pierre Nkurunziza hawezi kuwania muhula wa tatu. RFI/SR
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya elfu mbili wameandamana katika wilaya ya Musaga, kusini mwa mji wa Bujumbura, ikiwa ni mara ya kwanza idadi ya watu hao kushudiwa tangu kuanza kwa maandamano hayo wiki tatu zilizopita.

Katika wilaya ya Nyakabiga, raia wa Uganda wameungana na waandamanaji kwa siku ya leo Jumatatu. Viongozi wa maandamano hayo walijiunga na waandamanaji katika wilaya hiyo. Waandamanaji wamesema hawatositisha maandamano hadi pale Pierre Nkurunziza atakapo achana na mpango wake wa kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi ujao wa urais, unaopangwa kufanyika Juni 26.

Waandamanaji hawakujali onyo lililotolewa na Baraza la usalama la kitaifa nchini Burundi la kuwataka kusitisha maandamano, na kuondoa vizuizi barabarani.

Yale viongozi waliyotamka yanawahusu wao wenyewe, wala sio sisi. Tunachohitaji ni mabadiliko. Tutaendelea na maandamano haya hadi pale Nkurunziza atakapo achana na mpango wa kuwania muhula watatu ”, amesema mwanafunzi mmoja wa Chuo kikuu, ambaye alikua miongoni mwa waandamanaji.

“ Hatutaondoka barabarani, kwani Nkurunziza anaua watu, anapora mali ya nchi, anakiuka katiba ya nchi na Mkataba wa Amani wa Arusha. Hapa Burundi tunaishi kutokana na Mkataba wa amani wa Arusha. Kwa sasa raia kutoka jamii za Watuhu na Watutsi tunaishi pamoja, kwa hiyo tunapaswa kuishi kwa amani. Naye Nkurunziza anapaswa kuondoka”, amesema Florent, kijana mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni miongoni mwa waandamanaji.

Hayo yakijiri Ubelgiji imechukua uamzi wa kusitisha msaada wa Euro milioni mbili ambazo zingelipewa tume huru ya uchaguzi. nchi hiyo imesitisha pia msaada wa Euro milioni tatu uliyokua ukisaidia polisi. Ubelgiji inasema imechukua uamzi huo kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoshuhudiwa katika maandamano yanayoendeshwa na raia mjini Bujumbura, pamoja na kukaidi kwa rais Pierre Nkurunziza kwa kutowania muhula wa tatu. Uholanzi kwa upande wake imesema iko mbioni kuichukulia vikwazo Burundi.

Ubelgiji na Uholanzi ni nchi mbili za Ulaya ambazo zimekua zikisaidia polisi ya Burundi. Nchi hizi zinainyooshea polisi kuwakandamiza waandamanaji, hasa kuwauawa kwa risasi za moto waandamanaji 11 mjini Bujumbura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.