Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA

Watu kadhaa wauawa katika vurugu Bujumbura

Nchini Burundi, makabiliano mapya kati ya waandamanaji na polisi inayotuhumiwa na waandamanaji kushirikiana na vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd, Imbonerakure, yametokea Alhamisi wiki hii.

Nchini Burundi, umati wa waandamanaji ukiwafukuza wanajeshi wakiwatuhumu kutowalindilia usalama waandamanaji dhidi ya Imbonerakure na polisi , Mei 7 mwaka 2015.
Nchini Burundi, umati wa waandamanaji ukiwafukuza wanajeshi wakiwatuhumu kutowalindilia usalama waandamanaji dhidi ya Imbonerakure na polisi , Mei 7 mwaka 2015. RFI/SR
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na idadi iliyotolea na shirika la msalaba mwekundu, watu watatu wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa. Hata hivyo, guruneti imerushwa katika wilaya ya Kinama Kasakazini mwa mji wa Bujumbura na kugharimu maisha ya mtu mmoja na wengine saba kujeruhiwa. Wakati huo huo kulitokea makabiliano kati ya waandamanaji wanaopinga muhula watatu wa Pierre Nkurunziza na vijana kutoka chama tawala Imbenerakure, wanaomuunga mkono rais huyo.

Hali imeendelea kuwa tete katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bujumbura, hasa kufuatia mabadiliko katika mtizamo wa wanajeshi. Mpaka sasa jeshi limekua likipongezwa kwa kutoegemea upande wowote, lakini kwa sasa limeanza kunyooshewa kidole kwamba baadhi ya wanajeshi wameanza kuonekana kuwa wanaegemea upande wa chama tawala. Jeshi limekua likiondoa vizuizi viliyowekwa barabarani na waandamanaji katika wilaya ya Musaga, kusini mwa Bujumbura.

“ Baadhi ya wanajeshi wameanza kuonekana kuwa wanaegemea upande wa chama cha Nkurunziza “, wamesema waandamanaji wenye hasira.

“ Polisi inawalindia usalama vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd, Imbonerakure, na jeshi halina jukumu lolote”, wameendelea kusema waandamanaji hao.

Katika wilaya ya Nyakabiga, kijana mmoja aliyetuhumiwa kuwa mmoja wa vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd, Imbonerakure, ameuawa kwa kuchomwa moto.
Mawaziri wanne ikiwa ni pamoja na waziri wa usalama, wa ulinzi, wa mambo ya ndani na wa sheria wamejielekeza eneo la tukio, na kulani kitendo hicho.

■ AU yaomba kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais

Katika mahojiano na televisheni ya China ya CCTV, Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma ameomba uchaguzi wa urais uahirishwe nchini Burundi, akibaini kwamba hali ni tete zikisalia siku chache za uchaguzi.

“ Hatuwezi kwenda katika nchi kukutana na watu wakiitoroka nchi yao, na tusemi kuwa tutashiriki katika zoezi la uangalizi la uchaguzi”, amesema Dlamini-Zuma.

Umoja wa Afrika unapaswa kupeleka katika masaa arobaini na nane yajayo wanachama wake wa jopo la wazee wenye busara mjini Bujumbura. Umoja wa Afrika pia utawakilishwa katika mkutano wa kilele uliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hatima ya Burundi utakaofanyika mjini Dar es Salaam, Mei 13.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.