Pata taarifa kuu
MAREKANI-UN-TABIA NCHI

Trump kushinikiza kwa mageuzi ya Umoja wa Mataifa

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuhotubia mkutano wake wa kwanza wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Mataifa unaoanza jijini New York nchini Marekani.

Rais wa Marekani, Donald Trump, Septemba 15, 2017 katika uwanja wa ndege wa Morristown, kabla ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.
Rais wa Marekani, Donald Trump, Septemba 15, 2017 katika uwanja wa ndege wa Morristown, kabla ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Trump amekuwa akikosoa mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na kuuita kama kikao cha viongozi kukutana na kuwa na wakati mwema bila ya kutatua matatizo mbalimbali duniani.

Mzozo wa Korea Kaskazini, Iran na Mynmar itajadiliwa katika mkutano wa mwaka huu bila kusahau mabadiliko ya hali ya hewa na maswala ya usalama.

Huu ni mkutano wa kwanza pia kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guteress ambaye alianza kwa kuandaa mkutano wa kujadili mabadiliko ya utendaji katika Umoja huo.

Kabla ya kuhutubia Mkutano Mkuu, Donald Trump naye pia alihudhuria mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.