Pata taarifa kuu
UN-AFRIKA-USALAMA

Migogoro barani Afrika kujadiliwa kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mkutano maalum utafanyika kuhusu kikosi cha kimataifa katika ukanda wa Sahel (G5 Sahel) Jumatatu hii alasiri Septemba 18 mjini New York.

Marais wa nchi za G5 na Emmanuel Macron, tarehe 2 Julai 2017 mjini Bamako.
Marais wa nchi za G5 na Emmanuel Macron, tarehe 2 Julai 2017 mjini Bamako. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo watashiriki marais wa nchi tano, ikiwa ni pamoja na Emmanuel Macron, Alpha Condé, rais wa sasa wa Umoja wa Afrika, mkuu wa sera za kigeni wa Umoaj wa Ulaya na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Mkutano wa ngazi ya juu ambao utahimiza jumuiya ya kimataifa kuunga mkono kikosi cha pamoja cha kupambana na ugaidi wakati ambapo fedha zimekua ni mataitzo makubwa kwa utekelezaji wake.

Wakati ambapo G5 Sahel na Ufaransa wanataka kuona kikosi hiki kinafanya operesheni zake za kwanza mwezi Oktoba, bado kunakosekana robo tatu ya euro 423,000,000 zinazohitajika kuwa utekelezaji wake. Kwa hiyo ni mlolongo mzima wa kidiplomasia kwa kupata kifedha hizo. Kuna ulazima wa kushawishi jumuiya ya kimataifa na hasa Marekani ili kupata kuweza kupata kitita hicho katika mkutano huo mjini New York.

Kwa kukutanisha viongozi hawa wa ngazi ya juu, lengo ni kuonyesha kwamba nchi za zilizotoa askari wao katika eneo la Sahel (G5 Sahel), Ufaransa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa wanaamini kwa kauli moja umuhimu wa kikosi hiki na nia ya kukiunga mkono.

Haijulikani kama Marekani illioalikwa itashiriki katika mkutano huu na kama kweli itashiriki, kwa kiwango gani cha uwakilishi.

Siku ya Jumanne, semina ya kiufundi itawakutanisha pamoja wawakilishi wa wizara za ulinzi wa nchi zilizotoa askari wao katika eneo la Sahel (G5 Sahel) na Umoja wa Ulaya ili kufafanua na kutathimini mahitaji ya kikosi hiki.

Lakini mkutano wa New York unalenga hasa kuzindua uhamasishaji kabla ya mkutano wa wafadhili wa katikati ya mwezi Desemba utakaofanyika kando ya mkutano wa Baraza la Ulaya mjini Brussels, na sio katika nchi ya G5 kama ilivyopangwa awali, ili kuwezesha uwepo wa nchi nyingi na taasisi nyingi ziwezekanavyo.

Viongozi kadhaa wa nchi za Afrika wamewaili mjini New York kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Wana matumaini ya kusikilizwa wakati ambapo dunia in kabiliwa na migogoro mingi ya kimataifa.

Mbali na mkutano wa G5 Sahel, baadhi ya migogoro barani Afrika itachukua nafasi katika mkutano huo. Nchini Mali, pamoja na tukio la kipekee la mchakato wa amani bado limesimama.

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo rais Touadera, ataomba idadi ya askari wa Umoa wa Mataifa iongezwe nchini humo.

Migogoro nchini Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itajadiliwa zaidi kwa siri.

Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kukutana siku ya Jumatano wakati wa chakula cha mchana na Rais wa Marekani Donald Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.