Pata taarifa kuu
UN-UFARANSA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Trump na Macron kushiriki Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Emmanuel Macron anatazamia kuwasili New York kuhudhuria Mkutano wake wa kwanza wa Umoja wa Mataifa. Baada ya mlolongo mkubwa kabisa wa kimataifa tangu kuchukua hatamu ya uongozi, rais wa Ufaransa anaendelea na mkakati wake wa kidiplomasia.

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambapo viongozi kutoka duniani kote wanakutana wiki hii.
Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambapo viongozi kutoka duniani kote wanakutana wiki hii. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya kwanza ya emmanuel Macron katika Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne Septemba 19, yataruhusu kuweza kupata uhakikisho, kutoka kwa Donald Trump, kwa kutoa ujumbe mkali.

Kuzungumza na Umoja wa Mataifa ni kuzungumza na ulimwengu. Na ndivyo Emmanuel Macron atajaribu kufanya.Rais wa Ufaransa, ambaye atatoa hotuba yake ya kwanza siku ya Jumanne kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anataka kuelezea maana ya hatua ya Ufaransa katika ulimwengu, kuzungumza juu ya mambo mbalimbali, kuhamasisha suala la "mali ya pamoja" , kwa kifupi kutoa maono yake ya mahusiano ya kimataifa.

Maono ambayo yatafananishwa na ya yale ya Donald Trump, ambaye pia anachukua hatua zake za kwanza kwenye Umoja wa Mataifa. Kama ilivyo katika kundi la nchi zenye nguvu duniani (G7) mnano mwezi Mei au kundi la nchini zilizostawi kiuchumi (G20) mnamo mwezi Julai, Emmanuel Macron na Donald Trump wanatazamiwa kusikilizwa kwa makini katika kikao hiki ambacho kitarushwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa.

Wawili hao pia watakutana wakati rais wa Ufaransa atawasili New York. Lengo al mazungumzo hayo ni kuchukua hatua moja kwa moja kabla ya kikao hicho cha Umoja wa Mataifa, ambapo kutazungumziwa masuala nyeti kama uhusiano na Korea Kaskazini, hali inayoendelea nchini Syria, ugaidi, mazingira , mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Maswali ambayo Emmanuel Macron anatarajia kutoa mchango wake.

Lakini wawili hawa sio peke yao wanaoingia jikwaa la kimataifa la Umoja wa Mataifa. Pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anatazamia kushiriki kwa mara ya kwanza Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. "Nadhani kitakacho kuwa muhimu sio tu mapambano kati ya Macron na Trump, lakini kuwepo kwa Antonio Guterres," amesema mwanadiplomasia wa zamani Manuel Lafont Rapnouil, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa na mkurugenzi wa taasisi yaEuropean Council on Foreign Relations.

Emmanuel Macron na Antonio Guterres wanajua msimamo wa Donald Trump kuhusu mkataba wa hali ya hewa ulioafikiwa mjini Paris, nchini Ufaransa au kikosi cha amani cha Umoja wa Mataifa. Na licha ya kutokubaliana na rais wa Marekani, wote wawili wataepuka mapambano, ameeleza Manuel Lafont Rapnouil.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.