Pata taarifa kuu

Rais wa Ufaransa akutana kwa mara ya kwanza na rais wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amempokea Alhamisi, Mei 25, mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ubalozi wa Marekani mjini Brussels kwa ajili ya mkutano wao wa kwanza kabla ya mkutano wa muungano wa kijuhami wa chi za Magharibi (NATO). Viongozi hao wamechangia chakula cha mchana.

Rais wa Marekani Trump na mkewe wakimpokea rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ubalozi wa Marekani nchini Ubelgiji, Mei 25, 2017.
Rais wa Marekani Trump na mkewe wakimpokea rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ubalozi wa Marekani nchini Ubelgiji, Mei 25, 2017. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Kwenye ajenda ya mkutano wa Alhamisi hii, Mei 25 kati ya Donald Trump na Emmanuel Macron, ni mkutano wa muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO) na ule wa nchi zenye nguvu duniani (G-7), ambao utafunguliwa nchini Italia, migogoro ya kikanda (Syria, Ukraine, Korea ya Kaskazini. ..), uchumi na heshima, kwa utawala mpya wa Marekani kuhusu mkataba wa Paris uhusuo tabia nchi.

Baada ya kupeana mkono, Donald Trump kwa muda mrefu alimsifu rais wa Ufaransa, ambaye anamzidi umri wa miaka 30. "Ni heshima kubwa kwangu kuwa na rais mpya wa Ufaransa, ambaye aliongoza kampeni ya ajabu na alipata ushindi mkubwa," alisema rais wa Marekani Donald Trump. "Nina furaha kubwa pia kuwa na rais Trump," alisema Emmanuel Macron, "Nina furaha kubwa kwa kuweza kuketi pamaja na kubadilisha mambo mengi," aliongeza rais Macron.

Kutokana na muda mfupi wa mkutano huo uliofanyika katika chumba cha kulia cha Ubalozi wa Marekani, ikulu ya Elysee, siku ya Jumatano, ilisema inajiandaa kwa mazungumzo ya moja kwa moja na rais wa Marekani.

Hatua ya kwanza

Katika mkutano huo, upande wa Ufaransa, walikuepo Sylvie Goulard, Waziri wa Majeshi, Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Ulaya na Mambo ya Nje, Bernard Rogel, Mkuu wa majeshi katika ofisi ya rais na Philippe Etienne, Mshauri wa masuala ya Kidiplomasia wa Emmanuel Macron. Rais wa Ufaransa, aliyechaguliwa Mei 8 na kutawazwa Mei 14, kwa mkutano huo na mkutano wa NATO utaofuta, amepiga hatua yake ya kwanza katika masuala ya kimataifa ya kidiplomasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.