Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Donald Trump kuzuru Ufaransa kwa ziara ya saa 24

Rais wa Marekani Donald Trump anatazamiwa kuwasili Alhamisi Julai 13 nchini Ufaransa kwa ziara ya saa 24 ambapo atatumia muda mwingi pamoja mwenyeji wake Emmanuel Macron.

Donald Trump na mkewe Melania, wakiingia katika ndege  ya Air Force One kusafiri kwenda Paris Julai 12, 2017.
Donald Trump na mkewe Melania, wakiingia katika ndege ya Air Force One kusafiri kwenda Paris Julai 12, 2017. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Katika ajenda ya zira hiyo: mkutano wa pamoja na kuchangia chakula cha jioni katika mgahawa wa Mnara wa Eiffel Alhamisi hii, kisha gwaride la jeshi la Julai 14katika ikulu ya Champs Elysees siku ya Ijumaa. Kuepo kwa rais wa Marekani mjini Paris mwaka huu kunaendana sambamba na maadhimisho ya miaka 100 ya kuingia kwa Marekani katika Vita Kuu vya Dunia, pamoja na kwamba mwanzo wa uhusiano kati ya Trump na Macron ulikuwa ngumu na kuna masuala mengi ambayo hawafikiani.

Pamoja na uchovu wa safari mbili mfululizo barani Ulaya, Donald Trump pengine hafurahii ikiwa Washington itatengwa na marafiki zake.

Macron na Trump mwanzo uhusiano wao ulikua mgumu mwaka mmoja uliopita. Wawili hawa walikuwa wahaguliwa kwenye wadhifa wa juu baada ya kampeni zao za kwanza katika uchaguzi wa urais lakini mitazamo yao ni tofauti kabisa, na sio tu kwa sababu ya tofauti ya umri wao, ambapo Donald trump ana umri wa miaka 71 na Emmanuel Macron 39.

Nchini Marekani, Macron anaonekana kama mtu ambaye alisitisha kupanda kwa umimi katika nchi za Magharibi, wakati ambapo DonaldTrump na kauli mbiu yake ya "Marekani kwanza" ilionyesha kinyume. Wawili hawa kupeana mkono kwanza kulionekana kuna kuna tofauti fulani, Vile vile inafahamika kwamba wana migogoro kuhusu biashara ya kimataifa au auala la mazingira, ambapo Donald Trump alijitoa kwenye Mkataba wa Paris husu mabadiliko ya hali ya hewa.

Lakini hata kama wana mvutano huo, viongozi hawa wawili bado wanaonekana kuweka sawa uhusiano wao binafsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.